while loop hii ni aina ya loop ambapo code zitaendelea ku excute bila ya kikomo mpaka masharti ulioweka yatimie.
Tofauti na for loop, while loop hutumika sana kwenye maeneo haya:-
1. Hujui code zako zita excute mara ngapi mpaka kufikia matokeo.
Mfano ina program ya kuandika maudhui kwenye mafaili. Lengo lako unataka iandike MB 5, lakini hujui hizo code zita excute mara ngali mpaka ufikie MB 5. Hapa for loop haiwezi kufanya kazi.tutatumia while loop.
2. Una excute program yako kutokana na input za mtumiaji. Hapa kwa kuwa hatujui onput za huyo mtumiaji wako, hivyo tutatumia while loop.
Jambo lingine muhimu kulijuwa ni kuwa kwenye shule loop statement huweka mahala popote kwenye hiyo block.
Jinsi ya kuandika while loop.
Kwanza utaanza na initial ambapo inahitaji code zako zianzie ku excute.
while(condition){
Statement
}
Kuandika while loop ni rahisi sana yenyewe inahitaji condition na statement tu. Angalia mfano hapo chini:-
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
<body>
<script>
var a =0;
var watoto = ['juma', 'hassan', 'john', 'paul', 'rashidi', 'daudi', 'mwajuma'];
while(a < watoto.length){
document.write(watoto[a]+'<br>');
a++;
}
</script>
</body>
</html>
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
<body>
<script>
var a =0;
var namba = prompt();
while(a < namba){
document.write('Bongoclass'+'<br>');
a++;
}
</script>
</body>
</html>
Do while loop
Aina nyingine ya loop ni do while loop. Yenyewe ni kama while loop ila utofauti wake ni kuwa huwa inaanza kwanza ku excute code mara moja bila ya kujali shirti limefikiwa au bado. Endapo sharti limefikiwa basi itaendelea ku excute mpaka sharti limalizike. Na endapo halijafikiwa itastop.
Chukulia mfano huu
Tukichukuwa mfano wa hapo juu kama variable a tutaweka 11 code za hapo juu hazitafanya kazi. Ila kama tutatumi do while kwanza code zitafanyabkazi mara moja kisha ndipo itaanza kuangalia masharti. Kama yamefikiwa itaendelea kufanya kazi, vinginevyo I totally agree stop.
Kuandika do while
Kwanza utaanza kuweka do ikifuatiwa na mabano {} ndani ya mabano ndio utaweka statement yako ambayobitakuwa na increment ++ au decrement - - baada ya hapo ndipo utaanza kutest while
do{statement}
while()
Mfano
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
<body>
<script>
var a = prompt();
do{
document.write('Bongoclass'+'<br>');
a++;
}
while(a<10)
</script>
</body>
</html>
Endapo utaweka namba zaidi 10 utaona kwanza I ita excute mara moja.
Mwisho:
Huu ndio mwisho wa somo la condition statement. Tukutane somo linalofuata tutajifunza mambo kadhaa muhimu kabla ya kumaliza course.