JINSI YA KUWEKA VARIABLE KWENYE JAVASCRIPT.

Katika somo hili tutakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza variable kwenye javascript na kuweza kuzitumia. Pia tutaona kanuni zinazoambatana na variable kwenye javascript.

 

Je variable ni nini?

Variable ni kama chombo kinachohifadhia taarifa. Chukulia mfano una ndoo ambayo ndani yake ina maji, mikate, na mchele. Hapa ndoo ni variable ambayo inahifadhi. Ama mfano kusema x inawakilisha 8. hapa x ni variable ambayo inahifadhi 8.

 

Variable hutambulika kwa jina lake ambalo halitakiwi lijirudie tena kuwakilisha variable nyingine. Jina hili ni unique ambalo hutambulika kama identifier.  Variable inatakiwa iwe na zifa zifuatazo:-

  1. Jina hili linaweza kuwa na herufi, namba, underscore (_) na alama ya dola ($)
  2. jina lazima lianze na herufi au alama ya dola ($) au underscore (_)
  3. jina linatakiwa lizingatiwe matumizi ya herufi kubwa na ndogo. kwani katika javascript juma na JUMA ni majina mawili tofauti.
  4. majina yote ambayo ni javascript keyword hayaruhusiwi kwenye variable. Tumezungumzia kuhusu keyword kwenye somo lililotangulia.

 

Namna ya kuipa thamani javascript

Tunatumia alama ya = ili kuipa thamani variable. Kwenye javascript alama hii huitwa assignment operator na sio alama ya sawasawa kama ilivyo kwenye hesabu.

 

Kuna njia kuu tatu ambazo hutumika kwenye javascript ili kuipa variable thamani yake. Njia hizo ni kwa kutumia keyword kama:-

  1. var
  2. let
  3. const

 

1. Kwa kutumia var:

Hii hutumika pale unapotaka kuweka variable ambayo itaweza kutumiaka kwenye ukurasa mzima wenye block code nyingi yaani globally. Block code tulisha izungumzia katika masomo yaliyopita.

 

Mfano 1:

<script>

   var bc = "www.bongoclass.com";

   document.write(bc)

</script>

 

Hii itakupa matokeao haya:

Mfano 2

<script>

   var x = 2;

   var X = 3;

   document.write(x + X)

</script>

Hii itakupa matokeo haya

2. Kwa kutumia let

Let hutumika kuipa thamani variable ambayo itatumika kwenye block code moja tu yaani locally.

Mfano 3

<script>

   let web = "www.bongoclass.com";

   document.write(web)

</script>

 

Hii itakupa matokeo haya:-

3. Kwa kutumia const

Const pia hutumika kama ilivyo let, wote huipa thamani variable itakayotumika kwenye block moja ya code. utofauti uliopo katika ya let na const ni kuwa variable ya const huwezi kuirudia tena kwenye block nyingine.

Mfano 4:

<script>

   const blog = "blog.bongoclass.com";

   document.write(blog)

</script>

 

 

Variable nyingi kwenye statement moja

Pia unaweza kutumia variable zaidi ya moja kwenye statement moja kwa kutumia keyword moja, ila utataiwa kila variable uitengenishe na mwenzie kwa alama ya coma.

Mfano 5

<script>

   var embe = "dodo", samaki = "papa", mtihani = "hesabu",  web = "bongoclass";

   document.write(embe,  samaki, mtihani, web)

</script>

Hii itakupa matokeo:=

Hapo kuna changamoto kuwa maandishi yamebanana banana sana. katika somo linalofuata tutajifunza vyema namna ya kupangilia text out put kwenye javascript. Utajifunza namna ya kuachanisha hayo maandishi.

 

Variable isiyo na thamani (unidentified)

Endapo variable itatumika bila ya kupewa thamani. Variable hiyo italeta matokeo kuwa unidentified. Katika hali halisi unaweza kuacha variable bila ya kuipa thamani kwa malengo kuwa thamni yake itapatikana baada ya kukokotolewa baadaye ambba baada ya mtumiaji wa program atakapoweka thamani yake.

 

Mfan0 6

<script>

   let embe;

   document.write(embe)

</script>

 

hapo variable embe haijapewa thamanu yake hivyo kompyuta italeta matokeo kuwa haitambui thamni ya variable au unidentified. Angalia hapo chini

Mwisho:

Tukutane somo la 5 tutakapojifunza kuhusu mpangilio wa text output kwa kutumia javascript. Somo hili litakuhitaji angalau uwe unatambuwa tag za hatml kama <br>.