Ili uelewe vyema somo hili soma kwanza habari hii. Umetakiwa kusajili wanafunzi katika darasa la kwanza. Sharti mwanafunzi awe na umri kati ya miaka 6 hadi 8. Program itasema umefanikiwa kumsajili mwanafunzi Endapo mwanafunzi atakuwa na umri wa miaka chini ya 6 program inatakiwa iseme anatakiwa kurudi darasa la chekechea na endapo umri utakuwa zaidi ya miaka 8 basi program imwambie anatakiwa asome memkwa . Darasa letu litakuwa linachezea kwenye habari hiyo.


 

Condition statement ni nini?

Neno statement ni neno la kiingereza lenye maana maelezo na neno condition lina maana ya masharti. Hivyo kwa ujumla tunasema kuwa condition statement ni maelekezo ambayo yanakuwa na masharti. Maelekezo haya yanaweza kubeba pande mbili pande yabkwanza itabeba maelezo na pande ya lili itatupa matokeo.

 

Mfano: "endapo umri ea mtoto ni miaka 5". Haya ni maelekezo na matokeo yake anatakiwa kurudi darasa la chekechea. Hivyo shart hapa la kusajiliwa ni kuwa na umri kuanzia miaka 6.

 

Aina za condition statement:

Condition statement zipo katika aina kuu 3 ambazo ni:-

  1. if……else
  2. switch
  3. loop

Katika somo hili tutaona aina kwanza. Kisha switch na loop tutaisoma kwenye somo linalofuata.

 

  1. if…else

Tunataka tuanze kuona endapo umri wa mtoto utakuwa chinivya miaka 6.

Kwanza tutatiloa prompy() kwa ajili ya kudaka user input. Rejea somo la 15 tumezungumzia sana habari hii. 

Pili tutatumia variable kwa ajili ya ku store user input kutoka kwenye prompt(). Variable yetu tutaiita umri.  Hivyo code itasomeka hivi

let umri = prompt("Weka umri wa mtoto");

 

Tatu tutakwenda kutengeneza condition statement. Jinsfi ya kutengeneza condition statemen

  1. Utaanza na neno if 
  2. Litafuatiwa na mabano ()
  3. Ndani ya hayo mabano ndipo kunakaa mashart
  4. Kisha utaweka mabano mengine haya {} yanayifahamikabkwa jina la curl au brace
  5. Ndani ya jayo mabano {} utaweka maelekezo. Maelekezo haya yataonyesha nini kifanyike endapo sharti litatimizwa ama laa. 

 

Kwa mujibu wa mfano wetu,  shart amavcondition ni kuwa na umri kuanzia miaka 6. Ikiwa ni chini ya hapo program itatoa maelekezo. 

 

Kanuni ya kuandika if… else

 

if(weka sharti hapa){

weka maelekezo hapa

}

 

Kumbuka tayari tunayo vatiable yabkukusanya data ambazo zitajazwa. Variable hiyo ni umri rejea hapo juu. 

 

Sasa tunakwenda kusema kwenye shart ikiwa umri ni chini ya miaka sita. Kama tulivyoona hapo juu kuwa shart huwekwa ndanibya mabano (). Kumbuka alama hizi ambazo tulishasomaga masomo ya mwanzoni: -

> Kubwa kuliko

< Ndogo kuliko

== Sawa sawa na

=> Kubwa kuliko au sawa sawa na

<= Ndogo kuliko au sawa sawa na

& and au na hutumika kuunganisha mfano Juma na Ali

! hii hutumika katika kukanusha

|| hii hutumika kumaanisha au


 

Hivyo itaandikwa hivi: -

if(umri ) sas kwa kuwa umri tunaujuwa nibchini yabmiaka 6 tutasema if(umri < 6) hapo sharti limekamilika. 

 

Hatuwa inayofuata ni kuandika statement na kama nilivyotangulia kusema kuwa statement huandikwa ndani ya {} hivyo itakuwa hivi

 

if(umri <6){"Anatakiwa kurudi darasa la chekechea"} sasa kumbuka ili statement yetu ionekane tunatakiwa tutumie zile njia za ku onyesha matokeobya code kama document.write(). Hivyo code zetu zitasomeka hivi: -

 

if(umri <6){

document.write("Anatakiwa kurudi darasabla chekechea");}

 

Pia unaweza kitia rangi maandishi kwa kitumia html.  Kwa mfano hapo tutatumia <b style='color:blue'> Anatakiwa arudi darasa la chekechea</b>

 

Hivyo code nzima zitakuwa hivi: -

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  let umri = prompt("Weka umri wa mtoto");

if(umri < 6){

    document.write("<b style='color:blue'> Anatakiwa arudi darasa la chekechea</b>");

  }

</script>

  </body>

</html>

 

 

Sasa hapo utaona nimeweka namba 4 ambayo ni ndogo kuliko 6. Ukibonyeza ok utapata majibu haya. 



 

Kwa mfano huo huo sasa utaona kama utajaza umri kuanzia 6 na kuendelea haitaonyesha chochote. Sasa itatakiwa tuseme else yaani ukiwa umri ni zaidi ya mika 6 ama zsidi program iseme umefanikiwa kumsajili mwanagunzi. 

 

Kufanya hivi tutaongeza neno else baada ya mabano } kisha tutaweka mabano mengine {} ndani ya mabano haya tutaweka statement inayitakiiwa kuonekana endapo umribwa mtotobutakuwa miaka 6 ama zaidi. Hivyo code zitakuwa hivi 

if(umri < 6) {

statement

}else{

statement

}

 

Wacha tuone code 

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  let umri = prompt("Weka umri wa mtoto");

if(umri < 6){

    document.write("<b style='color:blue'> Anatakiwa arudi darasa la chekechea</b>");

  }else{

    document.write("<b style='color:purple'>  umefanikiwa kusajili mwanafunzi</b>");

  }

</script>

  </body>

</html>

 

Hapo utaona umri ni miaka 7 ambapo statement ya pili ndio itafanya kazi kutokana na sharti letu. Ukibofya Ok itakuletea matokeo haya

 

Jinsi ya kutumia else if

Ukirejea habari yetu inasema kuwa umri ukiwa zaidi yavmiaka 8 program itasema anatakiwa kusoma memkwa. Hivyo basi tunakwenda kuandika tena upya code zetu. Kwa kuweka masharti mawili. 

 

Kwa sharti la kwanza tutatumia if() na shartvla pili tutatumia if else() kanuni ni ileile baada ya mabank ya shart hufuatiwa na mabano ya statement. 

 

Kanuni inakuwa hivi

if(shart la kwanza){

statement

} else if(shart la pili) {

statement

}

 

Hakuna kikomo cha kuweka mashart unawezabkuweka masharti zaidi kwabkutumia else if

 Wacha tuone mfano wa code: 

 

Hatuwa ya kwanza 

Hapa tutaweka if() kama tulivyo anza mwanzo

if(umri < 6){

statement

}

 

Hatuwa ya pili ni kuweka sharti la pili

Sasa hapa ni sawa na kisema ikiwa umri ni zaidi ya miaka 5 ana ni chini ya miaka 9, inamaana tunachukuwa kuanzia miaka 5 hadi 8. Hapa tutatumia alama. Wacha tuone tutakavyoandika pamoja na lile shart la kwanza.

 

if(umri <6){statement

}else if(umri > 5 & umri <9){

statement}

 

Hatuwa ya tatu kwa kuwa tumeshamaliza kuweka mashrt sasa ni wakati wa kutumia else kwa maana ikiwa ni nje ya hayo mashrt program ifanye nini.

 

if(umri <6){statement 1

}else if(umri > 5 && umri <9){

statement 2}else{

statement 3}

 

CODE NZIMA ZIPO HIVI:

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  let umri = prompt("Weka umri wa mtoto");

if(umri < 6){

    document.write("<b style='color:blue'> Anatakiwa arudi darasa la chekechea</b>");

  }else if (umri >5 & umri < 9) {

    document.write("<b style='color:purple'>  umefanikiwa kusajili mwanafunzi</b>");

  }else{

    document.write("<b style='color:violate'>Anatakiwa kuanza memkwa");

  }

</script>

  </body>

</html>

 

Utaona hapo umri upo nje ya umri wa kujiunga na darasa la kwanza.

 

Kwa kutumia mfano huu inaweza kuweka sharti zisizo na idadi. Wacha tumalizie mfano huu hapa. Sasa tunataka ikiwa umri ni kuanzia miaka 18 program uilize je je ameoa ama kuolewa

 

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  let umri = prompt("Weka umri wa mtoto");

if(umri < 6){

    document.write("<b style='color:blue'> Anatakiwa arudi darasa la chekechea</b>");

  }else if (umri >5 & umri < 9) {

    document.write("<b style='color:purple'>  umefanikiwa kusajili mwanafunzi</b>");

  }else if(umri <18 & umri > 9){

    document.write("<b style='color:violate'>Anatakiwa kuanza memkwa");

  }else {

    document.write("<h1 style='color:red'>Je ameoa ama kuolewa?")

  }

</script>

  </body>

</html>

 

Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch.