Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu method ambazo hutumika kwenye namba na mahesabu yaani Math property na Number property. Kama ambavyo somo lililotangulia ulijifunza method zinazofanya kazi kwenye string. 

 

 

isInteger()

Hii hutumika katika kuthibitisha kama hiyo taarifa ni namba ama sio namba. Kama itakuwa ni namba itakupa jibu true na kama sio namba itakupa jibu la false

 

<script>

  var a=3, b="haloo";

document.write(Number.isInteger(a) +"<br>");

  document.write(Number.isInteger(b))

</script>

 

Utaona hapo variable a ni namba hivyo imekuja true na hiyo variable b imeleta false kwa kuwa sio namba.

 

 

isNaN()

Hii hutumika huthibitisha kuwa hiyo taarifa ilioingizwa sio namba. Huleta majibu ya true kama sio namba na false kama ni namba. 

<script>

  var a=3, b="haloo";

  document.write(isNaN(a) +"<br>");

  document.write(isNaN(b))

</script>

 

 

parseInt()

Hii hutumika kuchukuwa namba kutoka kwenye data iliyoingizwa. Kwa mfano unahitaji mtu aingize mwaka wake wa kuzaliwa kwenye program ambayo inauliza umri. Sasa unakuta ameandika hivi 26 ndio miaka yangu wakati alichotakiwa kuandika ni 26 tu. Hivyo Method hii itanyakuwa hiyo 26 na kuacha hizo zisizo husika. 

 

Medhod hii itachukuwa namba yeyote itakayokuwa mwanza. Kwa mfano ameandika 4 miezi na miaka 26 hapa itakayichukuliwa ni hiyo 4 hivyo program itatambuwa kuwa ana miaka 4.

 

Pia endapo ataandika hivi miaka 26 program haitatambuwa kitu. Kwa kuwa yenyewe inachukuwa character ya kwanza hivyo itakupa jibu NaN Angalia mfano hapo chini nimekuekea mitindo yotebhiyo. 

 

<script>

 

document.write(parseInt("26 ndio maka yangu")+"<br>");

  document.write(parseInt("4 miezi nabmiaka 26")+"<br>");

  document.write(parseInt("miaka yangu ni 26"))

</script>

 

parse    Float()

Hii hutumika kuchukuwa namba zenye viwango vya desimali kutoka kwenye string. Inafanana na hiyo ya hapo juu parseInt kuwa huchukuwa character ya kwanza, na huketa NaN kama imeanza na hefuri.

<script>

 

  document.write(parseFloat("56.6 kg")+"<br>");

  document.write(parseFloat("4.7 cm na futi 5")+"<br>");

  document.write(parseFloat("kilogram thelathini"))

</script>

 

toFixed()

Hii hutumika katika kukadiria viwango maalumu kwenye desimali. Kwa mfano namba hii 2.63698 tunataka kuiandika kwenye viwango viwili vya desimali hivyo itakuwa 2.64 utaona hapo imekuwa 4 baada ya kuikadiria na endapo tutaiandika kwenye kiwango kimoja itakuwa 2.6 kufanya hivi utatumia toFixed()

 

<script>

  var a=0.63698, b=2.63698, c=2.47290;

  document.write(a.toFixed(0) +"<br>");

  document.write(b.toFixed(1) +"<br>");

  document.write(c.toFixed(2))

</script>

 

toExponential()

Hii hutumika kubadili namba iliyo katika viwango vya desimali kwa katika exponent. Hivyo kuiandika namba ki sayansi zaidi. 

 

<script>

  var a=32.63698, b=2.63698, c=2432.47290;

  document.write(a.toExponential(1) +"<br>");

  document.write(b.toExponential(2) +"<br>");

  document.write(c.toExponential(3))

</script>

 

 

toString()

Hii hutumika katika kubadili namba kuwa string. Kwa mfano ukiweka namba hii 24 program itatambuwa hii namba kama string hivyo itaichakata hii namba kama "24" kisha kuirudisha matokeo yake kama 24 ila utofauti ni kuwa hatambuliki tena kuwa ni namba ila ni string .

 

<script>

  var a=32, b=24, c=243;

  document.write(a.toString()+"<br>");

  document.write(b.toString()+"<br>");

  document.write(c.toString())

</script>

 

 

ceil()

Hii hutumika katika kukadiria viwango vya desimali round up kwa maana kuwa bila kujali kwamba ni kubwa kuliko 5 yenyewe itaongeza moja kwenye namba husika. 

<script>

   document.write(Math.ceil(3.76353)+"<br>");

  document.write(Math.ceil(1.239)+"<br>");

  document.write(Math.ceil(0.13))

</script>

Katika matumizi ya kawaida chukulia kuwa unakokotoa ni watu wangapi wanaweza kupita kwenye daraja husika kwa wakati mmoja. Sasa unapata jibu kuwa ni watu 2.3 kiuhalisia hapo inamaana watu 2 na kidogo. Sasa ni vyema kitaalamu useme ni watu watatu ndio wanapita hapo.  Hivyo tunapuuzia desimali zilizopo na kuweka 3. Ina maana kuwa hatuna shaka kabisa kuwa watu watatu watapita. 

 

floor()

Hii hutumika kukadiria namba kwa kupuuza viwango vyote vya desimali vilivyopo na kulibakisha nmab yenyewe. Kwa mfano 6.9 hii itasomeka 6 bila kujali viwango vya desimali. Hii ndio kitaalamu huitwa roun down

<script>

  document.write(Math.floor(3.76353)+"<br>");

  document.write(Math.floor(1.239)+"<br>");

  document.write(Math.floor(0.13))

</script>

 

Katika matumizi ya kawaida mfano unataka kulipa wafanyakazi lakini katika mahesabu yako mfanyakazi atatakiwa kulipwa Tsh 424900.28 hivyo hapa tutatumia floor na kuondoa hizo .28 na kwa mahesabu haya mfanyakazi atapokea 424900

 

round()

Hii sasa ndio ile namna ya kukasirika ambayo tuneizoea kuwa inaangalia kama namba inayofuata ni 5 ama zaidi utaongeza moja. Vinginevyo utawacha. 

<script>

 

  document.write(Math.round(3.76353)+"<br>");

  document.write(Math.round(1.4539)+"<br>");

  document.write(Math.round(0.13))

</script>

 

sqrt()

Hii hutumika katika kutafuta Square root ya namba. Mfano 10 *10 = 100 kitaalamu huitwa kipeuo cha pili katika mfano huo namba 10 ni kipeuo cha pili cha namba 100 hivyo 10 ni square root .Method huu huchukuwa namba ambazo ni positive endapo itakuwa negative italeta jibu NaN .wacha tuone mifano. 

<script>

 

  document.write(Math.sqrt(100)+"<br>");

  document.write(Math.sqrt(9.9)+"<br>");

  document.write(Math.sqrt(-25))

</script>

 

cbrt()

Hii hutumika kupata cubic root of a number yaani kipeuo cha tatu. Kwa mfano 

<!DOCTYPE html>

<html>

<head>

   <title>cubic root</title>

</head>

<body>

   <p id="demo"></p>

 

   <script>

      var a = Math.cbrt(8);

      var b = Math.cbrt(1000);

      var c = Math.cbrt(15.625);

      var d = Math.cbrt(-27);

      

      document.getElementById("demo").innerHTML =

      a + "<br>" +

      b + "<br>" +

      c + "<br>" +

      d;

   </script>

</body>

</html>

 

max()

Hii hutumika katika kupata namba kubwa kutoka kwenye orodha ya namba. Kwa mfano kati ya 4, 2, 1 na -9 ni namba gsnibkubwa kuliko nyingine. Hapo namba kubwa ni 4 

<!DOCTYPE html>

<html>

<head>

   <title>Namba kubwa</title>

</head>

<body>

   <p id="demo"></p>

 

   <script>

      var a = Math.max(3, 27,21, 1, 45, 3, -234, -560);

      var b = Math.max(-1, -8, -13, -2, -13);

      

      document.getElementById("demo").innerHTML =

      a + "<br>" +

      b;

   </script>

</body>

</html>

Main()

Hii ni kinyume na Max hii yenyewe inaleta namba ndogo kuliko zote. 

<!DOCTYPE html>

<html>

<head>

   <title>Namba ndogo</title>

</head>

<body>

   <p id="demo"></p>

 

   <script>

      var a = Math.min(3, 27,21, 99, 45, 3);

      var b = Math.min(-1, -8, -13, -2, -13);

      

      document.getElementById("demo").innerHTML =

      a + "<br>" +

      b;

   </script>

</body>

</html>

pow()

Hii hutumika kutafuta thamani ya namba itakayozidishwa kwa vipeo kitaalamu inaitwa power.  Kwa mfano 5² au 4³ sasa hapo hiyo 5 na 4 huitwa base na 2 na 3 huitwa power. 

 

Hivyo 5² ni sawa na kusema 5*5 ambapo ni sawa na 25. Na hiyo 4³ ni sawa na kusema 4 *4*4 ambapo ni sawa na 64.

 

pow() itakuwa na parameter mbili ambapo ya kwanza ni base na ya pili ni power. 

<script>

  document.write(Math.pow(5, 2)+"<br>");

  document.write(Math.pow(4, 3)+"<br>");

</script>

 

 

abs()

Chukulia mfano unataka watu wawe wanaingiza namba kwenye program. Tuseme mtubatatakiwa kuingiza umri wake. Sasa kuna mwingine akaingiza -17 kumaanisha ana miaka 17 lakini hiyo namba ni negative hivyo haitahesabika ni 17 katika program. Hivyo basi tutatakiwa kuzifanya namba zote hizi ni sawa kwa kutumia abs ili tupate absolute number .

 

<script>

  document.write(Math.abs(5)+"<br>");

  document.write(Math.abs(-8)+"<br>");

</script>

 

random()

Hii itatusaidia kutengeneza rondom namba. Kila uki run code itakuletea namba tofauti na ile ya kwanza namba hii ndio tunaziita random number. 

<script>

  document.write(Math.random()+"<br>");

</script>

 

Kila uki run hizo code utapata namba nyingine. Sasa changamoto ya hapo ni kama unavyoona hizo namba zimeanza na desimali. Sasa ikiwa unataka isiwe na desimali utatakiwa kutumia floor() kisha unazidisha kwa 10 mfano Math.floor(Math.random() * 10) hii hapa kwanza ita zidisha kwa 10 hiyo random namba kisha ita round down jibu ili kupata nzima. Hivyo namba zitacheza kati ya 0 na 9.

<script>

  document.write(Math.floor(Math.random() * 10));

  

</script>

 

Sasa ikitokea unataka zaidi ya hapo tuseme nataka random namba zitokee kati ya 10 mapaka 100 tutazidisha kwa 100. Na kama unataka iwe kati ya 100 na 1000 utazidisha kwa 1000. Na zaidi mfano

<script>

  document.write(Math.floor(Math.random() * 1000000));

  

</script>

 

Mwisho

Tukutane somo la 13 tutakwenda kujifunza kuhusu method ambazo zinatumika kwenye array. Vyema kujifunza vyema kuhusu array kabla ya kuingia kwenye somo.