AINA ZA DATA ZINAZOTUMIKA KWENYE JAVASCRIPT
Aina za data ambazo javascript inatumia ni sawa na zile ambazo zinapatikana kwenye programming language nyingine kama php. Javascript inatumia aina zifuatazo:-

Namba
javascript ni tofauti na programming language zingine kama php ambapo namba kuna zenye desimali na zisizo. Kwenye javascript namba ni namba iwe na desimali ni namba ama isiwe na desimali.
Mfano 1:

Itakupa matokeo haya:

String
String ni mkusanyiko unaojumuisha namba, herufi na alama. Aina hii inachukuwa amala zote, namba zote na herufi zote. Mfano ukisema “bongoclass” hii ni string. Au ukisema “admin5@bongoclass.com” hii pia ni string ambayo ina namba, 5 alama @ pamoja na herufi. Kumbuka string siku zote inakaa ndani ya alama za kufunga na kufungua semi, kama ilivyo mifano hapo juu.
Mfano 2

Hii itakupa matokeo haya:-

Boolean
Kama ilivyo kwenye programming language zingine, bulean inabeba matokeo mawili tu true au false. Ainahii ya data pia hutumika kwenye javascript. Tulishaona mifano kadhaa katika somo lililotangulia wakati tunajifunza namna ya kutumia logic.
Mfano 3
Tunaelewa kuwa 3 ni kubwa kuliko 2. Hivyo tunatarajia itupe jibu la true kuwa ni kweli tatu ni kubwa kuliko mbili.

Mfano 4
Tunaelewa kuwa 5 ni kubwa kuliko 4 sasa endapo tutaandika 4 ni kubwa kuliko 5 inatakiwa itupe majibu false yaani sio kweli kuwa 4 ni kubwa kuliko 5.

Array
Array ni mkusanyiko wa data za aina moja ambazo huweza kufikiwa kwa jina moja. Katika javascript pia tunatumia array. Siku zote array huanzia na 0. Kwa kuwa ni mkusanyiko wa data, basi ile ya kwanza kutajwa hupewa namba 0. Na pia array siku zote hukaa ndani ya mabano [], na kila moja inakuwa ndan ya alama ya kufunga semi kama zilivyo string. Na kama list ina item nyingi kila moja hutenganishwa kwa alama ya koma ( , ). Angalia mifano hapo chini
Mfano 5:

Kama nilivyokueleza kuwa array huanzia na 0 hivyo basi katika array hapo juu 0 ni mpapani, 1 ni muembe, na 2 ni muarobaini. Na endapo unataka kuisoma array ya 2 basi baada ya kutaja array utaweka mapbano na kuweka 2.
Mfano 6:

Object
Object ni data ambayo inakuwa na sifa pamoja na aina. Object inakuwa na jina na thamani, ikitenganishwa na alama ya coma. Pia object huandikw ndani ya mabano ya curly {}.
Mfano 7:

Hapo utaona kuwa object wetu ni tovuti, ambaye ana sifa hizo hapo, jina, url, status na umri. Hivyo data zilizo katika aina hii huitwa object. Mfano mwingine wa Object ni kama
Mfano 8:

Jinsi ya kujuwa aina ya Data iliyotumika:
Ili kujuwa aina ya data iliyotumika hapa tunatumi javascript keyword inayoitwa typeof Mfano tunajuwa “juma” ni string na 5 ni namba. Hivyo tunataka kuziweka hizi data ili tujuwe ni aina gani ya data.
Mfano 9:

Undefined na empty
Kwenye javascript kama umeweka variable lakini hukuipa thamani hiyo huitwa undefined. mafano kuandika let x; hii itakupa jibu undefined variable.
Na endapo umeweka variable lakini ukaipa thamani hewa hiyo huitwa empty. Kwenye javascript data hii hutambulika kama string. mafano kusema let y = “”; hii ni empty haileti chochote lakini hutambulika kama string.
Mfano 10:

Tukutane Somo linalofata tutakuja kujifunza kuhusu javascript functions, na jinsi zinavyofanya kazi.