avascript ni moja ya programming language ambazo hutumika sana katika kutengeneza web page na program nyingine. Javascript ni lugha muhinu na ya lazima kuijuwa kama unataka kutengeneza website ili na ubora. Kwenye ukurasa wa wavuti kazi kuu ya javascript ni kuweka tabia mbalimbali za ukurasa huo, kama kuweka kazi za batani pindi mtu anapobofya batani.
Sifa za mwenye kujifunza:
Ilikushiriki vyema course hii unahitajika uwe na uelewa na html. Angalau uwe umeshiriki mafunzo ya HTML leve 1 itakuwa vyema zaidi ukiwa umemaliza level 2. Course hii itaanza mwanzo mpaka mwisho, na imelenga zaidi kwa wale ambao ndio kwanza wameanza kujifunza javascript.
Maandalizi ya kifaa chako kwa ajili ya kujifunza
Javascript inafanya kazi kwenye HTML. yaani tutatumia ukurasa wa HTML ili kujifunza javascript. Hivyo hakuna maandalizi zaidi kwa level hii, maandalizi ni kama yale ambayo umeyafanya kwenye kuandaa kifaa chako ulipokuwa najifunza html.
Historia ya javascript:
Javascript imevumbuliwa na Brendan Eich mnamo mwaka 1995. Ilianzishwa kwa ajili ya Netscape 2 na baadaye ikachukuliwa na kampuni ya ECMA-262. Kutoka hapo javascript ilipitia mabadiliko mengi na matoleo mengi.
Nini javascript hufanya kwenye ukurasa wa wavuti?
-
Inaweza kubadili maudhui kabisa ya ukurasa wa wavuti na kuweka maudhui mapya baada ya kufanya kitendo husika.
-
Javascript inaweza kubadili thamani za attribute kwenye ukurasa wa wavuti (angalia html level 2 kujifunza zaidi kuhusu html attributes)
-
Javascript inaweza kubadili style ya ukurasa wa wavuti
-
Javascript inaweza kufisha ama kuonyesha element flani ya html (rejea mafunzo ya html level 2 kujifunza zaidi kuhusu html element)
Vipi javascript hutumika kwenye ukurasa wa html?
Ili kuweza kutumia javascript kwenye ukurasa wa html unatakiwa utumie tag za javascript. Tag ya javascript ni . Nadani ya tag hii ndipo hukaa code za javascript. Mfano:
Hii itakupa matokeo “hujambo javascript” angalia picha hapo chini.
Wapi tag za javascript hukaa kwenye ukurasa wa html?
Unaweza kuweka popote pale, kwenye
ama
ila ni vyema script kuziweka kwenye
kisha function zake kuweka pale inapohitajika kwenye ukurasa. Hii husaidia kuboresha mpangilio na muonekano wa code zako. Tutajifunza zaidi jambo hii mbele.
Umuhimu wa kujifunza javascript programming language:
-
Utaweza kuifanya website/blog yako kuwa na tabia njema na muonekano mzuri
-
Unaweza kutengeneza dynamic website kwa kutumia javascript library kama react
-
Javascript inaweza kutumika ku access database kwa kutumia library kama node
-
Javascript ni programming language itakayokusaidia katika kufanya project mbalimbali kama kwenye game, web App, desktop App n.k
-
Javascript hutumika kuimarisha security kwenye website na blog.
-
Kama unataka kutengeneza geme kwa kutumia html, basi javascript huwezi kuiepuka.
Je wajuwa kuwa:
-
Facebook inatumia react ambayo ni library ya javascrip, wanatumia hii kwa ajili ya mtandao mkubwa wa facebook. Wanatumia javascript kuifanya facebook kuwa kama unavyoiona leo.
-
Google hutumia javascript kwenye bidhaa zao kama gmail, google doc, firebase n.k. Mtandao mkubwa wa firebase kwa ajili ya kuhost website na App database unatumia javascript. Kwa kutumia firebase unaweza kuwa na database yako ambayo hutumia javascript kuaccess data zako, ku update na kufuta.
-
Mirosoft ni kampuni nyingine inayotumia javascript kwenye shughuli zao. Kuna makampuni mengine yanatuia javascript kwenye baadhi ya huduma zao.
-
Paypal
-
Linkedin
-
Walmart
-
Uber
-
eBay
-
Capital one
-
Citibank
Tukutane somo linalofuata ambapo tutaanza kujifunza namna ya kuandika javascript na kuona matokeo yake.