MATENDO YA KIHESABU

Somo hili litakwenda kukujulisha namna ya kutumia matendo ya kihesabu katika javascript. matndo ya kihesabu ni muhimu sana katika kutengeneza program za kikompyuta. 

 

Katika program za kihesabu alama za matendo ya kihesabu huitwa operator na namba ambazo hutumika kwenye hesabu huitwa operand.

 

Matendo ya kihesabu (operator) ni kama:-

  1. Kujumlisha +

  2. kutoa -

  3. kigawanya /

  4. kuzidisha *

  5. modulus % hii hutumika kwenye kugawanya na kubakia

  6. increment ++

  7. decrement –

 

1. Kujumslisha

Kama tulivyoona hapo juu kujumlisha namba tunatumia alama ya jumlisha ambayo ni +. 

 

Mfano 1

<script>

   var a = 4

   var b = 5

   var c = a + b

  document.write(c)

</script>

 

hii itatupa matokeo ya 9

 

Pia unaweza kutumia alama hii ya kujumlisha kuunganisha string zaidi ya moja. String ni mkusanyiko wa namba na herufi ama herufi tupu. Angalia mfano wa hapo chini

 

Mfano 2

<script>

   var a = 'juma';

   var b = 'Ali'

   var c = a + b

  document.write(c)

</script>

 

hii itakupa matokeao haya

Utaona neno juma na Ali yameungana kutengeneza jumaAli. Katika hali ya kawaida ya kiuandishi yanatakiwa yasomeke juma Ali kwa kuacha nafasi katikati yao. katika javascript ktatuwa changamoto hii tutatumia alama ya kujumlisha +” “ + angalia mfano hapo chini:-

 

Mfano 3

<script>

   var a = 'juma';

   var b = 'Ali'

   var c = a +" "+ b

  document.write(c)

</script>

 

Hii itatupa matokeo haya

Pia unaweza kujumlisha string na namba. Angalia mfano hapo chini

 

Mfano 4

<script>

   var a = 'bongo';

   var b = 5;

   var c = a  + b;

  document.write(c)

</script>

 

Hi itatupa matokeo haya:

Mfano 5

<script>

   var a = '7';

   var b = 5;

   var c = a  - b;

  document.write('Jibu ni' + " "+ c)

</script>

 

Hii itakupa matokeo haya

Katika mfano huo hapo juu jibu 75 yaa ni 7 na 5 na sio namba sabini na tano. Ni kwa sababu namba 7 imetumika kama string na ndio maana utaiona ipo ndani ya alama hizi '7'   

 

2. Kutoa

Ili kutoa namba tunatumia alama ya - kama inavyotumika kwenye hesabu. Utaweza kutoa namba kubwa kutoa ndogo, ama nndogo kutoa kubwa na jibu litakuja kwenye negative yaani hasi. Angalia mifano hapo chini

 

Mfano 6

<script>

   var a = '7';

   var b = 5;

   var c = a  - b;

  document.write('Jibu ni' + " "+ c)

</script>

 

Hii itatupa matokeao

Mfano 7

<script>

   var a = 5;

   var b = 9;

   var c = a  - b;

   document.write('Jibu ni' + " "+ c)

</script>

 

Hii itatupa matokeo haya:-

Huwezi kutoa namba na herufi ama herufi na namna. ukifanya hivi itakupa error. Analia mfano hapo chini 

 

Mfano 8

<script>

   var a = 5;

   var b = 'haloo';

   var c = a  - b;

   document.write('Jibu ni' + " "+ c)

</script>

 

Hii itakupa matokeo haya

3. Kuzidisha

Tunatumia alama hii * kuzidisha namba. Angalia mifano hapo chini

 

Mfano 9

<script>

   var a = 5;

   var b = 4;

   var c = a * b;

   document.write(c)

</script>

 

hizi zitakupa matokeo haya:-

4. Kugawanya

Ili kugawanya namba tunatumia alama ya kugawanya ambayo ni . Angalia mofano hapo chini:

 

Mfano 10

<script>

   var a = 20;

   var b = 4;

   var c = a / b;

   document.write(c)

</script>

 

 

Hii itakupa matokeo haya:-

Endapo utagawanja na itabadi badi itaendelea kugawanya na kukupa jibu kwenye desimali.

 

Mfano 11

<script>

   var a = 10;

   var b = 3;

   var c = a / b;

   document.write(c)

</script>

 

Hii itakupa jibu:-

 

Pia unaweza kujuwa namba iliyobaki wakati wa kugawanya. Kwa mfano 10 ukagawa kwa 3 jibu ni tatu na kubakia moja. Sasa ukitaka kujuwa namba iliyobaki utatumia alama hii % tofauti na kutumia . Alama hii % inaitwa modulu. Angalia mfano hapo chini:

 

Mfano 12:

<script>

   var a = 10;

   var b = 3;

   var c = a % b;

   document.write(c)

</script>

 

Jibu hapa litakuwa ni 1 kama ilivyo hapo chini

Mwisho: 

Tukutane somo la 7 tutakwenda kujifunza alama za kihesabu katika kulinganisha yaani logic. Somo la 7 litakuwa muhimu sana kwa ambao wana malengo ya kuja ku code software na web App. Alama nyingine mbili za ++ na – tutajifunza katika masomo yanayokuja.