Katika somo hili utajifunza kanuni za kuandika code za javascript ama javascript statement.Lamda kwanza nianze kukujuza maana ya hili neno statement. Ni kuwa kwenye program ya kikompyuta kuna code amabazo ni maelekezo ambayo kompyuta hupewa ili kufanya jambo fulani. Sasa hizi code ama haya maelekezo ndio huitwa statement.

 

Katika somo hili utajifunza kanuni za kuandika hizi statement. Kanuni hizi zitaweza kukuongoza kwa ufupi uweze kugunduwa kama kwenye code zako kuna tatizo. Na kama lipo nini kimesababisha. Hivyo tutajifunza syntax ya javascript.

 

Kabla hujasonga mbele zaidi na somo hili, nikujuze kuwa javascript statement inaweza kuwa na vitu hivi Values, Operators, Expressions, Keywords, na Comments. Value ni thamani ambazo zinaweza kuwa ni thamani za variable, operator ni alama za kihesabu kama + kumaanisha jumlisha, Expression ni mkusanyiko wa variable, value na operator, na comment hapa ni sehemu ambayo programmer ama mtu anayeandika hizo code kuweka kumbukumbu zake, ili baadaye aweze kukumbuka.

 

Kanuni za kuandika javascript:

  1. Matumizi ya semicolon (;)

Weka alama hii ya semicoloni mwishoni mwa ststement yako. kwa mfano:

Mfano: 1

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="demo"></p>

 

<script>

   let x, y, z;

   x = 5;

   y = 6; 

   z = x + y;

 

   document.getElementById("demo").innerHTML =

       "The value of z is " + z + ".";

</script>

 

</body>

</html>

Hapo juu utaona mwishoni mwa kila msitari kuna alama ya semicolon. Pia unaweza kuunganisha statement nyingi katika msitari mmoja na kutenganisha kwa semicoloni. 

Mfano 2

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="demo"></p>

 

<script>

   let x, y, z; x = 5; y = 6; z = x + y; document.getElementById("demo").innerHTML = "The value of z is " + z + ".";

</script>

 

</body>

</html>

Matokeo ya statement ya kwanza, na ya pili ni sawa, ijapokuwa hii ya pili ina mistari kidogo ya code, ni kwa saabu imeunganishwa pamoja na kutengenishwa kwa alama ya semicolon kwa kila statement.

 

  1. Kuruka nafasi wakati wa uandishi (White Space):

Ni kuwa wakati unaandika huwa tunaruka nafasi, huwenda zikawa nyingi ama moja. Sasa katika javascript nafasi ambayo itahisabika kwenye code ni moja tu, hizo ambazo umeongeza javascript hazita zitambuwa na hasita athiri matokeo ya code zako. 

 

Hivyo unaweza kuruka nafasi kadiri uwezavyo, ili kuweza kuboresha muonekano wa code zako. Angalia mifano ya code hizo hapo chini majibu yake ni sawa.

Mfano 3

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="demo"></p>

 

<script>

    document.getElementById("demo").innerHTML = "haloo javascript";

</script>

 

</body>

</html>

Mfano wa 4

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="demo"></p>

 

<script>

    document.getElementById        ("demo").       innerHTML             =           "haloo                   javascript";

</script>

 

</body>

</html>

  1. Urefu wa msitari wa code

urefu wa msitari wa code hauwezi kuathiri matokeo ya code. Hata hivyo inashauriwa usizindi character 80. Inashauriwa pia kupunguza urefu wa msitari wa code kwa kuukata msitari (line break) baada ya semicoloni (;) kama ilivyo kwenye mfano wa kwanza huko juu.

 

  1. Uandishi wa code block

Hiki ni kifungu cha javascript statement, ambapo kuna statement zaidi ya moja, katika kundi moja. Kwa kutumia block unaweza kukusanya statement nyingi katika kundi ila wakati wa kufanya kazi huwa inaanza mojamoja kama zilivyo katika mpangilio. Kila statement itatenganishwa na semicolon.

Mfano 5

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<button type="button" onclick="myFunction()">Click Me!</button>

 

<p id="demo1"></p>

<p id="demo2"></p>

 

<script>

   function myFunction() {

       document.getElementById("demo1").innerHTML = "haloo statement 1";

       document.getElementById("demo2").innerHTML = "Hi statement 2";

   }

</script>

 

</body>

</html>

Ukibofya hiyo batani hapo utaona matokeo ya statement mbili ambayo moja itakuwa ni demo1 na nyingine ni demo1. ambapo zote zipo kwenye block moja ya function iliyoitwa myFunction()   

 

  1. Matumizi ya keyword

Code za javascript huanza na keyword

Keyword haya ni maneno maalumu ambayo yapo kwenye kanuni za uandishi za javascript. Maneno haya yanakuwa tayari yapo na huwezi kuyabadili. kwenye javascript kuna zaidi ya maneno 63 ambayo ni keywords. mifano ya keywords ni var, let, const, if, switch, for, function, return, try

           

  1. kuweka comment

comment ni muhimu sana katika uandishi wa code. Comment itakusaidia kukumbuka ama watu wengine kujuwa nini hasa msitari wa code unamaanisha. code zote zilizomo kwenye comment hazihusiki katika ufanyajikazi wa program.

 

ili kuandika comment utatumia // kama comment ni msitari mmoja au /*comment */ kama comment iitakuwa ni zaidi ya msitari mmoja.

Mfano 6:

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

<p id="myP"></p>

 

<script>

   //Mfano wa comment ya msitari mmoja";

   document.getElementById("myP").innerHTML = "My first javascript file";

   /* mfano wa koment wa

misitari mingi */

</script>

 

</body>

</html>

 

  1. case sensitivity:

javascript ni case sensitivity, yaani ukibadili herufikubwa na ndogo itakuwa ni shida. Unatakiwa uamuwe kama unatumia herufi kubwa ziwe kubwa na kama ni ndogo ziwe ndogo. Yaani B na b ni vitu viwili tofauti. Hivyo kama una variable B na kisha ukatumia b kama ndio variable yako hapa utapata error

Mfano 8

<!DOCTYPE html>

<html>

<body>

 

 

<p id="demo"></p>

<p id="demo2"></p>

 

<script>

   let B, b;

   B = "bongo";

   b = "class";

   document.getElementById("demo").innerHTML = B;

   document.getElementById("demo2").innerHTML = b;

</script>

 

</body>

</html>

Hapo ukifunguwa hilo file kwenye browser utapata matokeo mawili tofauti, ijapokuwa variable ni sawa lakini zina utofati, moja ni herufi kubwa na ingine ni herufi ndogo.

 

  1. Unadishi wa Camel Case

Camel case ni namna ya kuunganisha maneno kwenye code. Kuna aina nyingi za kufanya hivi kwa mfano kwa kutumia  alama hii - inayofahamika kwa jina la hyphen mfano background-color au kwa kuchanganya herufi kubwa na ndogo mfano FirstName  au kwa kutumia alama hii _  inayofahamika kwa jina la underscore mfano last_name  na zipo njia zinginezo.

 

katika javascript tunatumia style inayoitwa lower camel case hapa tunaanza na herufi ndogo, kisha kama kuna jina tunaliunganisha litaanza nanherufi kubwa. Mfano firstName, lastName, masterCard, interCity. 

 

Tukutane somo la 4 tutakapokuja kujifunza namna ya kuandaa variable kwenye javascript na kuweza kuitumia.