Somo leu moja kwa moja linakwenda kuanzia kwenye code za hello world. Copi code hizo hapo chini kisha pest kwenye text editor unayotumia.
fun main() {
println("Hello World")
}
1. Kotlin file extension
Format ya faili ya Kotlin ni kt. Mfano faili linaloitwa mafunzo litaandikwa hivi mafunzo.kt .kwa wale ambao mnatumia jetbrain faili lako utaliona kwenye folda linaloitwa kotlin. Angalia upande wa kushoto kuna palipoandikwa scr bofya hapo kisha bofya main kisha bofya kotlin hapo utalikuta faili lako. Kuanzi hapo ndipo tunapoendelea kufanyia mazoezi.
2. Mwanzo wa program
Kama ukiangalia ode hizo hapo juu utaona program yetu imeanza na keyword fun, hii keyword ama hili neno hutumika katika kuandika function. Funnction ni kikundi cha code ambazo huweza kutumika kufanya kazi fulani. Tunajifunza zaidi huko mbele.
Kisha utaona kuna keyword nyingine main() hii ndio function yenyewe. Hii huonyesha mwanzo wa program ya kotlin. Function hii code zake zipo ndani ya {}. Kwa mfano utaona hapo kuna println(“hello world”). Hapo kuna function nyingine ya println() hii hutumika ku print matokeo ya code kwenye screen.
Sasa ili kuona matokeo bofya batani ya kijani iliyofanana na batani ya kuplay mziki, inapatikana kwa juu katikati hii ni kwa wanaotumia kompyuta na software ya jetbrain. Kwa wale wanaotumia simu bofya batani ya ku play ama fuata maelekezo ya App unayotuia. Na kama unatumia online compiler weka code kusha bofya run.
Kisha angalia kwa chini itakuwa inaonyesha kama ina run. Ikimaliza unaona neno hello world kwenye ubao mweusi kwa chini. Huo unao ndio unaitwa console angalia picha hapo chini namba 3. Namba 1 inaonyesha neno java hapa nataka utambuwe kuwa kotlin yenyewe inafanyakazi kwenye java environment na hapo kwenye namba 2 utaona kuna 0. Hiyo inaonyesha kuwa code zime run bila hata ya matatizo.
Kama unatumia software nyingine maelekezo hayo hapo juu unaweza kuwa tofauti.
Katika matoleo ya zamani ya Kotlin ulihitajika kuweka parameter kwenye main function ambapo mfano wa hapo juu utaandikwa hivi
fun main(args : Array<String>) {
println("Hello World")
}
3. String na nmba
String ni mkusanyiko wa herufi, namba, na alama nyinginezo. Mfano mafunzo_55@bongoclass.com . Sasa unapoandika string utatakiwa kutumia alama ya (“) yaani quotation mark ama alama za kunukuu. Hivyo itaandikwa “mafunzo_55@bongoclass.com” kama hutoweka hizo alama haitaweka ku run. Ama kuhusu namba huna haja ya kuweka hizo alama. Na endapo utaziweka haitahesabika ni namba ila itakuw ani string ijapokuwa itaonekana ni namba. Angalia mfano hapo chini
fun main() {
println("mafunzo_55@bongoclass.com")
println(4)
}
4. Matumizi ya semicolon (;)
Katika kotlin semicolon sio lazima kama ilivyo kwenye lugha nyingine ila unaweza kuweka kama ukitaka.. Hata hivyo kama unataka kuunga statement utaitumia. Kwa mfano code hizo hapo juu ukitaka kuziandika kwenye mstari mmoja, hapo utaweka semicolon ili kutengenisha statement mbili. Statement ni kikundi cha code kinachofanya kazi fulani.
fun main() {
println("mafunzo_55@bongoclass.com") ;println(4)
}
Hapo kama hutaweka hiyo semicolon program hairaweza ku run, itakuletea error
5. Escape character (backlash)
Sasa kuna changamoto endapo unataka kuandika kifungu cha kunukuu, hutoweza tena kutumia alama za kunukuu yaani funga semi na fungua semi (“”) kwa sababu ukizitumia zinaingiliana na code za kotlin. Hivyo kutatuwa tatizo hili utatumia backlash kwa ajili ya ku escape character angalia sentensi hii (Amesema Mtume “Mwenyezi Mungu ni Mmoja”)
fun main() {
println("Amesema Mtume "Mwenyezi Mungu ni Mmoja"")
}
6. Line break yaani kukata mstari
Endapo utahitaji kukata mstari utatumia alama hii
fun main() {
println("Bongoclass Google Facebook Youtube")
}
7. commenting
Comment ni maelezo ya ziada abayo anaweza programmer kama kumbukumbu kwa ajili ya siku zijazo. Comment hazihusiki kwenye ku run program. Hivyo comment haiathiri program ufanyaji kazi wake.
Tunatumia alama ya // yaani double slash kwa ajili ya kuweka comment mstari mmoja. Na kama comment ina mistari mingi tutatumia slash kisha nyota /* hapo ni kufunguwa kisha ukimaliza comment utaweka nyota kisa slash */. Angalia mfano hapo chini:-
fun main() {
//hii ni comment ya mstari mmoja
println("Bongoclass Google Facebook Youtube")
/*hi ni comment ya
mistari zaidi ya mmoja
kwenye Kotlin
*/
}
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza khusu jinsi ya kutengeneza variable kwenye Kotlin.