Library ni nini?
Library ni mkusanyiko wa maelekezo ya programu, yaani ni yale maelekezo ambayo huamuru kompyuta kuyafuata. Kotlin yenyewe ina library zake. Kwa mfano, wakati tunajifunza kuhusu mahesabu, tulitumia library ya math ambapo tuli import kwa kutumia `import kotlin.math`.
Hizi library zipo nyingi na kila moja ina matumizi yake mengi tu. Kwa muda wako, unaweza kuzifuatilia Kotlin library kwenye tovuti yao ya jetbrain, link nimeitoa kwenye somo la kwanza.
Jinsi ya kutengeneza library yako mwenyewe.
Ili uweze kutengeneza library, kwanza utatengeneza faili nyingine kisha utalipa jina unalolotaka. Kwa mfano, tutatengeneza faili tutaiita `hesabu.kt`.
Ndani ya hilo file mstari wa kwanz akabisa tutatengeneza package name. Kwa mfano library yetu itakuwa kwenye package ya mylib. Hivyo tutaandika hivi package com.mylib.hesabu
Utaona hapo nmeanza keyword package ikafuatiwa na jina la hiyopackage ambalo ni com.mylib.hesabu baada ya hapo utaanza kuandika code zako library.
Sasa, chukulia tunataka library yetu ya hesabu iweze kufanya mambo kama kutafuta eneo la pembe tatu, eneo la mraba, na eneo la trapeza. Tutatumia kanuni za darasa la 5 shule ya msingi. Eneo la pembetatu ni (kimo * kitako) / 2, eneo la mtatili ni (urefu * upana), na eneo la trapeza ni ((a + b) * h / 2).
Sasa, kanuni hizi kila moja wapo hapo, tutazitengenezea function yake ili kuweza kufanya kazi husika. Kisha weka code kwenye faili letu tuloliita hesabu.kt .
package com.mylib.hesabu
fun pembeTatu(kimo: Int, kitako: Int): Double {
return (kimo * kitako) / 2.0
}
fun eneoMraba(urefu: Int, upana: Int): Int {
return urefu * upana
}
fun eneoTrapeza(a: Int, b: Int, h: Int): Double {
return ((a + b) * h / 2.0)
}
Mpaka kufikia hapa library yetu itakuwa imekamilika. Kilichobaki ni kuitumia kwenye faili letu la code.
Sasa ili tuweze kuitumia library yetu tutaanza na ku import library kwa kutumia package name yake na kuzingatia function tunayotaka kuitumia.
import com.mylib.hesabu.pembeTatu
import com.mylib.hesabu.eneoMraba
import com.mylib.hesabu.eneoTrapeza
fun main() {
val triangleArea = pembeTatu(5, 8)
val rectangleArea = eneoMraba(4, 6)
val trapezoidArea = eneoTrapeza(3, 5, 7)
println("Eneo la pembetatu: $triangleArea")
println("Eneo la mstatili: $rectangleArea")
println("Eneo la trapeza: $trapezoidArea")
}
Kwa namna kama hiyo, unaweza kutengeneza library yako ili kuwezesha utendaji kazi wa project yako.
Mwisho:
Huu ndio mwisho wa somo letu, katika somo linalofuta tutajifunza Object Oriented Programming yaani OOP.