Tulisha jifunza kuhusu string katika somo la aina za data. Pia tulijifunza mambo kadhaa khusu string kama interpolation na concatnate. Katika somo hili tutaingia ndani zaidi.
String indexing
Katika programming unaweza kuitumia character yeyote kwenye string husika. Kwa mfano katika string bongoclass hapo naweza kusoma herufi moja moja. Tunapohesabu index ya string tunaanza na 0. Hivyo katika string Bongoclass kama tunataka kusoma herufi ya mwanzo tu hapo tutatumia index ya 0
Mfano:
fun main() {
val text = "Bongoclass"
print(text[0])
}
Hapo utaona imeleta B
fun main() {
val text = "Bongoclass"
print(text[6])
}
Hapa itakuletea l
Sas kwa mfano unataka kujuwa kwenye string yetu ya bongoclass neno class linapatikana kuandia index ya ngapi. Kufanya hivi tutatumia indexOf .
fun main() {
val text = "bongoclass"
print(text.indexOf("class"))
}
Hapo itakupa jibu 5 kumaanisha kuwa neno class kwenye string ya bongoclass hupatikana kuandia index ya 5, kumbuka tunahesabu index kuanzi 0.
Kujuwa idadi y character kwenye string (string length)
Kwa mfabo tunataka kujuwa katika string bongoclass kuna character ngapi. Hapo tutatumia length property.
Mfano:
fun main() {
val text = "Bongoclass"
print(text.length)
}
Hapo itakuletea jibu 10 kumaanisha kuwa kuna character 10.
Kubadili string kuwa katika herufi kubwa na ndogo
Kama unataka kubadili string case kutoka herufi kubwa kwenye ndogo utatumia lowercase() na kama unataka kubadili kutoka ndogo kuwa kubwa utatumia uppercase()
Mfano:
fun main() {
val text = "bongoclass"
val text2 = "BONGOCLASS"
println(text.uppercase())
print(text2.lowercase())
}
Kulinganisha string mbili:
Wakati mwingine utahitaji kulinganisha string mwili. Kama zipo sawa. Kufanya hivi utatumia compareTo. Ikiwa itakupa jibu 0 ujuwe zipo sawa, na ikikupa jibu tofauti ujuwe hazipo sawa.
Mfano:
fun main() {
val text = "bongoclass"
val text2 = "bongoclass"
print(text compareTo text2)
}
Hiyo itakupa jibu 0.
Kuunganisha string zaidi ya moja:
Tulisha jifunza kuhusu concatnate, hapa tutarejea tu kidogo kw akutumia mifano miwili.
fun main() {
print("bongo" + "class")
}
Hiyo itakupa jibu bongoclass
fun main() {
val a = "bongo"
val b = "class"
print(a + " "+ b)
}
Hiyo itatupa bongo class
Kutumia variable kwenye string
Tulisha jifunza kuhusu interpolation pia kwa jina jingine huitwa string template. Hii ni njia inayotumika katika kutumia variable na statmenet nyingineo kwenye string
Mfano:
fun main() {
val search = "Google"
val social = "facebook"
val video = "youtube"
print("kuna aina nyingi za webite kama vile search engine ambayo ni ${search.uppercase()} socila network website kama $social na pia kuna video mmedia website kama $video ")
}
Jinsi ya kupata random string
Random string ni string inayotengenezwakutokana na set ya string, ila inakuw aimechanganya changanywa. Kufanya hivi tutatumia random
Mfano:
fun main() {
val text = "bongoclass"
print(text.random())
}
Hapo itakuwa inakupa herufi tofauti tofauti bila ya mpangilio. Ila hapo itakupa character moja tu. sasa ikitokea unahitaji kupata character zaidi ya moja utatakiw akuweka range yako maalumu. Kwa mfano tunataka kutengeneza character 5.
fun main() {
val str = "bongoclass"
for (i in 1..5) {
print(str.random())
}
}
Hapo ita generate string yenye character 5. Njia hii unaweza kuitumia katikaku tengeneza password.
Mfano:
fun main() {
val str = "abcdefghijklmnopqrstuvwxyzABCD@$#*123456789"
var password = ""
for (i in 1..12) {
password += str.random()
}
println(password)
}
DC7#rr7@2gCs
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu if else, else if.