Kama ilivyo kwa baadhi ya language kama Kotlin inatumia keyword var na val katika kuandika variable. Variable ni kiwakilishi ni nacho hifadhi thamani fulani ya data. Kwa mfano nikisema x ni sawa na 4 yaani (x = 3) hapa tunasema kuwa x ni variable ambayo inahifathi thamani ya 3.
Sasa tukija kwenye Kotlin tukitaka kuandika variable x kuwa inawakilisha 3 hapo tutatumia keyword var au val. Lamda kabla hatujakwenda mbali nikujulishe kuwa keyword i maneno maalumu ambayo hutumika kwenye language husika.keyword ni kama fun, main, var, val tunaendelea kuziona keyword nyingine kadiri somo linavyokwenda.
Ili uweze kuandika variable kwanza utaanza na keyword var ama val kisa utafuatia kuandika jina la hiyo variable yaani identifier kisha litafuatiwa na alama ya (=) kisha ndipo utaweka thamani ya hiyo variable. Neno thamani tutalitumia kama value.
Mfano:
fun main(){
var x = 3
val y = 4;
}
Sawa wacha tuone mfano haisia. Tunataka kujumlisha namba 4 na 3 kwa kutumia variable zao. Angalia mfano hao chini:
fun main(){
var x = 3
val y = 4
var ujumbe = "Mfano wa variable"
print(ujumbe + ' ')
println(x +y)
}
Utofauti wa var na val
Unapotumia val kutengeneza variable, hiyo variable unaweza kuibadilishia thamani. Mfano variable yetu x = 3, tunataka kuibadilishia thamani kuwa 4. Kubadilisha thamni ni kuitengeneza variable upya kwa jina lilelile.
fun main(){
var tovuti = "Bongoclass"
tovuti = "Google"
println(tovuti)
}
Hii ita output Google;
Mfano kama huo huwezi kuufanya kwa kutumia val.
Sheria za uandishi wa jina la variable:
- Variable haianzi na namba
- Unaweza kuanza na herufi, alama ya dola $ ama underscore (-)
- Zingatia matumizi ya herufi ubwa na ndogo, kama variable ina herufi ndogo hata unapokuwa unaitumia uweka ndogo kama ilivyo
- Kuwezi kutumia reserved keyword mfano var, String
- Ukitaka kuu nganisha majina mawili kuwa moja tumia niia ya camelCase yaani yaunganishe pamoja ila kila moja uanze kuliandka kwa herufi kubwa. Mfano jitu refu variable hii itaandikwa JituRefu hata hivyo unaweza kuandka vyovyote ila tu haitakiwi kuacha nafasi
- Huruhusiwi kuacha nafasi.
Concatnation na interpolation
Concatnation ni kuunganisha, hapa tunatumia alama ya (+) ili kuunganisha variable mbili angalia mgfano hapo chini:
fun main(){
var b = "Bongo"
var c = "class"
print(b + c)
}
Interpolation ni kuitumia variable ndani ya string. Hapo utaanza kuandika alama ya dola $ ikifuatiwa na mabano {} ndani ya mabano weka hiyo variable. Angalia mfano hapo chini:
fun main(){
var b = "Bongo"
var c = "class"
print("${b + c} ni muunganisho wa maneno mawili ambayo ni ${b} na ${c}")
}
Mwisho:
Katika somo linalofuata utakwenda kujifunz akuhusu data type yaani aina za data kwenye Kotlin.