Method ni nini?
Method ni kama function, lakini tofauti ni kuwa method zina uhusiano mkubwa na object. Hapa nitakuletea baadhi ya method za String:-
String length
Hii hutumika kujuwa je, string ina herufi ngapi.
fun main() {
val text = "haloo bongoclass"
println(text.length)
}
Hii itakupa jibu 16, kumaanisha hapo kuna herufi (character) 16.
Kubadili herufi kuwa ndogo au kubwa
Kubadilisha kuwa herufi ndogo utatumia toLowerCase na kubadilisha kuwa kubwa utatumia toUpperCase.
fun main() {
val text1 = "haloo bongoclass"
val text2 = "HALOO BONGOCLASS"
println(text1.toUpperCase())
println(text2.toLowerCase())
}
HALOO BONGOCLASS
haloo bongoclass
Kuigawa string kwenye (substring)
Kwa mfano, katika neno "bongoclass," tunataka kuchapisha neno "bongo" tu.
fun main() {
val text = "bongoclass"
println(text.substring(0, 5))
}
bongo
Kuchuja string (contains)
Kwa mfano, unahitaji kuangalia kama neno fulani lipo au halipo kwenye string.
Kama lipo, utapata jibu true, na kama halipo, jibu ni false. Wacha tuangalie je neno "class" lipo kwenye neno "bongoclass"?
fun main() {
val text = "bongoclass"
println(text.contains("class"))
}
true
Kubadili string kuwa list data type (split)
Hapa tutakwenda kuigawa string kwenye mafungu. Kwa mfano, neno "haloo karibu bongo class." Tutagawa kwa kila neno.
fun main() {
val text = "haloo karibu bongoclass"
println(text.split(" "))
}
Kubadili list kuwa string (join)
fun main() {
val text = listOf("haloo", "karibu", "bongoclass")
println(text.joinToString(" "))
}
haloo karibu bongoclass
Kuangalia je string imeanzia ama kuishia na neno fulani.
Kwa neno "karibu bongoclass," tutakwenda kuangalia je string imeanza na neno "bongoclass." Kama kweli, jibu ni true, na kama si kweli, jibu ni false.
fun main() {
val text = "karibu bongoclass"
println(text.startsWith("bongoclass"))
println(text.endsWith("karibu"))
}
false
false
Kuondoa nafasi za ziada (trim)
fun main() {
val text = " karibu bongoclass "
println(text)
println(text.trim())
println(text.trimStart())
println(text.trimEnd())
}
Kubadili sehemu ya string
Kwa mfano, badala ya kusema "karibu bongoclass," tunataka kubadili neno "karibu" kuwa "kwaheri."
fun main() {
val text = " karibu bongoclass "
println(text.replace("karibu", "kwaheri"))
}
kwaheri bongoclass
Mwisho
Method nyingine nyingi zipo. Hivyo, unaweza kuzitafuta kwenye mafunzo mbalimbali. Katika somo lifuatalo, tutajifunza method ambazo hutumika kwenye nambari.