Kukadiria namba 

Chukulia mfano 10/3 = 2.5. Sasa tukiikadiria hapa tutapata 3. Kufanya hivi tutatumia method ya roundToInt(). Kwanza tuta import math library. Library hii inahusu mahesabu tu. tunakuja jifunza zadi jinsi ya kutengeneza library yetu wenyewe masomo yanayofuata.

 

import kotlin.math.roundToInt

 

fun main() {

   val jibu: Double = 10.0 / 4.0

   println(jibu)

   println(jibu.roundToInt())

}


 

Kuangalia sifa za namba yani properties:

Namba shufwa (isEven)

Hii itatoa jibu true ikiwa kweli na false ikiwa si kweli. Tutashtua kama 4 ni shufwa

fun main() {

   val isEven: (Int) -> Boolean = { it % 2 == 0 }

   println(isEven(4))

}


 

Kutengeneza hashcode ya namba (hashCode)

Hii itakuletea hashcode ya namba husika. Kwa mfano, neno “bongoclass”  tunakwenda kuitengenezea hashcode

fun main() {

   val number = "bongoclass"

   println(number.hashCode())

}

 

2084316335

 

Kunagalia kama namba ni hasi tutatumia isNegative

Kuangalia kama namba ni infinit - haina mwisho tutatumia isInfinit

Kuangalia kama namba ni finit - ina mwisho tutatumia isFinite

Kuangalia kama namba sio negative - hasi tutatumia isNan

Kuangalia kama namba ni witiri yaani odd tutatumia isOdd

fun isInfinit(number: Double): Boolean = number.isInfinite()

 

fun isFinite(number: Double): Boolean = number.isFinite()

 

fun isNan(number: Double): Boolean = number.isNaN()

 

fun isOdd(number: Int): Boolean = number % 2 != 0

 

fun main() {

   val number = 4.0

 

   Check conditions for a Double

   println(isInfinit(number))

   println(isFinite(number))

   println(isNan(number))

 

   Check condition for an Int

   println(isOdd(4))

}

 

Kubadili namba kuwa string toString

fun main() {

    println(4.toString())

}

 

Zipo method nyingine za namba. Sasa nataka tuhame tuingie kwenye library ya math yaani math library.

 

Math library

Ni mkusanyiko wa tools za kufanyia mahesabu. Tutakwedna kujifunza vyema katika somo la library. Hapa ninachotaka ni uweze kujifunza kuitumia library ya mahesabu.

 

Kwanza tutatakiwa ku import hii library kama tulivyofanya kwenye kotlin.math. Ku import math library tutatumia import kotlin.math kisha utaweka jina la hiyo function unayoitaka kwa mfano kama ni power itakuwa import kotlin.math.powKisha library itakuwa tayari kuweza kutumiwa.

 

Mfano 1:

Tunataka kutafuta 2 kipeuo cha tatu yaani 2 power 3 (2^3). Kufanya hivi tutatumia pow()

import kotlin.math.pow

fun main() {

    println(2.0.pow(3.0))

}

Hapo itakupa jibu 8. Ambapo ni sawa na kufanya 2*2*2

 

Mfano 2

Tuna namba mbili 2 na 3, sasa tunataka kutafuta namba kubwa ni ipi na ndogo ni ipi. Hapa tutatumia min() na max()

import kotlin.math.min

import kotlin.math.max

fun main() {

    println(max(2, 3))

    println(min(2, 3))

}

 

Mfano 3:

Tunataka kutafuta square root ya namba, kwa mfano 49 ambapo ni sawa na kusema 7 * 7 = 49

import kotlin.math.sqrt

fun main() {

    println(sqrt(49.0))

}

 

Mfano 4:

Unataka kufanya hesabu za logarithm, sasa unataka kujua log ya 25

fun main() {

   val result = Math.log(25.0)

   println(result)

}

3.2188758248682006

 

import kotlin.math.log10

 

fun main() {

   val result = log10(25.0)

   println(result)

}

1.3979400086720377

 

Kuna mengi unaweza kuyapata kwenye math library. Kwa kuwa umeshajua jinsi ya kuitumia, unaweza kuitafuta kupitia website ya Kotlin, link yake utaipata kwenye somo la kwanza.

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata tutakwenda kuziona method nyingine ambazo zinafanya kazi kwenye list data type.