Operator hizi ni alama ambazo hutumika katika kufanya matendo mbalimbali kwenye variable ama thamani mbalimbali. Mfano 10 + 5, katika mfano huu 10 na 5 huitwa operand na hiyo alama ya kujumlisha (+) huitwa operator. 

 

Kwenye Kotlin operator zimegawanyika kama:-

  1. Arthmetics operator
  2. Assignment operator
  3. Comparison operator
  4. Logical operator

 

Arithmetics operator:

Hizi ni operator ambazo hufanya kazi kwenye matendo ya kihesabu. 

  1. Kujumlisha (+) mfano 5 +8
  2. Kutoa (-) mfano 7 -5
  3. Muzidisha (*) mfano  2 *3
  4. Kugawanya (/) mafno 6 /3
  5. Modulus (%) hii huonyesha namba inayobaki wakati wa kugawanya mfano 10%3 hapo jibu ni 1, kwa kuwa ndio inayobaki
  6. Increment (++) hii huongeza namba 1 kwenye namba ya mwanzo.

Mfano:

fun main() {

   var a = 2

   ++a

   print(a)

}

 

Hapa jibu ni 3 kwa kuwa imeongeza 1 kwenye namba ya mwanzo.

 

  1. Decrement (- -) hi hupunguza 1 kwenye namba ya mwanzo.

Mfano:

fun main() {

   var a = 3

   --a

   print(a)

}

 

Hapo jibu ni 2 kwa kuwa imepunguza 1 mwenye namba ya mwanzo.


 

Assignment operator:

Hizi ni zile operator ambazo hutumika ku assign thamani kwenye variable, yaani kuipa variable thamani. Kama unaposema var x = 2 hapo assignment operator (=) imetumika kuipa x thamani yake. 

Mifano ya assignment operator:-

  1. Alama ya (=) mfano a = 3
  2. Alama ya (+=) mfano a += 3 hii ni sawa na kuandika a = a+3
  3. Alama ya (-=) mfano a -=3 hii ni sawa na kuandika a = a-3
  4. Alama ya (*=) mfano a *=3 hii ni sawa na kundika a = a *3
  5. Alama ya (/=) mfano a /=3 hii ni sawa na kuandika a = a/3
  6. Alama ya (%=) mfano a %3 hii ni sawa na kuandika a = a %3

 

Comparison operator:

Hizi ni operator ambazo hutumika katika kulinganisha yhamani mbalimbali. Na zenyewe ni katika data type ya boolean yaani zinatoa jibu la true  ama false. 

  1. Equal to yaani sawa sawa na (==) mfano 5==7 hii ina maana kuwa 5 ipo sawa na 6 hapa jibu ni false
  2. Not equal yaani sio sawa (!=) mfano 5 !=7 hii ina maana 5 sio sawa na 7 hivyo jibu ni true
  3. > greater than yaani kubw akuliko (>) mfano 5>4 hapa ni true
  4. Less than yaani ndogo kuliko (<) mfano 5<4 hapa ni false
  5. Greater than or eaqual to yaani kubwa kuliko au sawasawa (>=) mfano 6 >=8 hapa ni true 
  6. Less than or equal to yaani ndogo kuliko au sawasawa na (<=) mfano 6<=6 hapa ni true

 

Logical operator:

Hizi hutumika kuweka logical kwenye variable ama thamani

  1. && huitwa logical and alama hii kwenye programming inamaanisha and yaani “na” . yenyewe italeta jbu true kama statement itakuwa kweli na kinyume chake. Mfano 2 ni kubwa kuliko 1 na 3 kubwa kuliko 2. Sasa haya melezo yote ni sawa hivyo jibu ni true. Maelezo haya unaweza kuyaandika hivi:  2 > 1 && 3>2

 

  1. || huitwa logical or alama hii ina aana or  yaan “au” hii itatoa jibu true kama moja ya statement ni kweli mfano 2 ni kubwa kuliko 5 au 6 ni kubwa kuliko 5. Hapa statement ya kwanza sio kweli, lakini ya mbili ni kweli, hivyo kwa ujumla tutapata jibu true kwa kuwa moja ya statement ni true. Maelezo haya tunaweza kuyaandika hivi 2 > 5 || 6>5

 

  1. ! huitwa logocal not kazi yakeni kukataa statement, kama ni ya ukwei inakuwa ni uongo. Mfano tunajuwa kuwa 5 ni sawa na 5 hivyoukiandika hivi 5 ==5 hi ni true. Lakini kama nitaweka logical not itamaanisha 5 sio sawa na 5 yaani 5 !=5 hapa jibu litakuwa ni false kwa kuwa sio kweli.

 

fun main() {

  print(5!=5)

}

 

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata utakwenda kujifunza kuhusu String kwa undani zaidi.