Katika somo lililopita tulijifunza jinsi ya kutengeneza variable bila ya kutaja aina ya data kwenye hiyo variable mfano var x = 6. Ila wakati mwingine utahitaji aina maalimu ya data ndio itumike. Kwa mfano kwenye user input. Hivyo hapa itatubidi tutaje aina ya data kwenyehiyo variable. Mfano var x: int 6;
Kama ukiangalia huo mfano vyema utaona kwanza nimetumia keywor ya kutengeneza variable. Unaweza kutumia yeyote kama ni var au val. Kisha utaweka jina la variable likifuatiw na nukata pcha (:), kisha ndipo utaweka type ya data.
Aina za data kwenye Kotlin:
- Number yaani namba
- Characters
- Booleans
- String
- Array
- Namba:
Kwenye kotlin bado namba imegawanyika katika makundka kama:
- Byte: Hizi ni namba nzima zinazoanzia -128 na kuishia 127
- Short: Hizi huanzia -32768 hadi 32767
- Int: hizi huanzia -2147483648 hadi 2147483647
- Long: hizi huanzia -9223372036854775807 hadi 9223372036854775807
Hizo ni namba nzima ambazo hazipo kwenye desimali. Na zile za decimali nazo zimegawanyika kama:-
- Float hii hubeba namba yenye viwango vya desimali 6 ama 7
- Double hii hubeba naba yenye viwango vya desimali mapaka 15
Katika hizi namba za float na double pia kuna scientific namba hizi ni aba ambazo zipo kwenye power of 10
Mfano:
fun main(){
val x: Float = 2E3F
val y: Double = 3E2
println(x)
println(y)
}
fun main(){
val x: Float = 0.9876F
val y: Double = 3.09
println(x)
println(y)
}
Ili kuitofautisha double n float. Kwenye float utaweka F mwisho angalia hapo juu.
fun main(){
val z = 12; //Byte
val x = 2147483647 // Int
val y = 2147483648 // Long
println(z)
println(x)
println(y)
}
2. Boolean
Hizi ni data ambazo zipo katika namba mbili tu ambazo ni true na false. Edha iwe sawa ama sio sawa. Mfano ji kwenye switch ya umeme, kama haitakuwa ni OFF basi itakuwa ON.
fun main(){
val x: Boolean = true
println(x)
//namba 5 ni sawa na 4? hii sio kweli
print(5 ==4)
}
- character:
Hapa tunakwenda kuangalia matumiazi ya char. Kwenye programming char ni character moja mfano a ama b ama c. Tofauti na String ambayo huwekwa kwenye (“”) double quort hizi char huwekwa kwenye (‘’) single quirt. Mfano:
fun main(){
val x: Char = 'V'
println(x)
}
- String
String ni mkusanyiko wa herufi,namba, alama za uandishina mengineyo. String huandkw akwenye double quort (“”).
fun main(){
val jina: String = "Bongoclass"
println(jina)
}
- Array
Hii ni data ambayo inaweza kukusanya data zaidi ya moja kwenye variable moja.
fun main(){
val web = arrayOf("Bongoclass", "Youtube", "Facebook", "instagram")
println(web[0])
}
Jinsi ya kubadili aina ya Data:
Sasa kuna wakati mwingine utahitajikubadili aina mojaya data kwenda aina nyingine. Kufanya hivyo tutatumia function hizi:-
- Kwenda Byte tutatumia toByte()
- Kwenda Short tunatumia toShort()
- Kwenda Int tutatumia toInt()
- Kwenda long tutatumia toLong()
- Kwenda float tutatumia toFloat()
- Kwenda double tunatumia toDouble()
- Kwenda char tunatumia toChar()
fun main(){
val x: Int = 5
val y: Long = x.toLong()
println(y)
}
Hapo jibu ni 5 ijapokuwa namba niilelile lakini sasa sio int ila ni long.
Mwisho:
Katika somolinalofuata tutakwenda kujifunzakuhusu operator.