JINSI YA KUPANGILIA MAANDISHI WAKATI WA KU OUT PUT JAVASCRIPT

Katika somo lililotangulia tulikutana na shida moja kuwa maandishi yametoka yakiwa yamebanana banana. Sasa katika somo hili tutajifunza namna ya kupangilia muonekano wa maandishi.

 

Njia zinazotumika kupangilia muonekano wa maandishi:

  1. Kwa kutumia html tag 

Kwa kutumia html tag unaweza kupangilia muonekano wa text zako kwa namna utakayo. Angalia mfamo hapo chini:-

 

Mfano 1

<script>

   document.write('<p style="color:blueviolet">Haloo bongoclass</p>');

</script>

Hii itakupa matokeo haya

Unaweza kufanya mengi kwa kutumia html ili kupangilia muonekano wa maandishi kwenye javascript. Lakini hebu tuangalie namna ambavyo mfano unaofuata utakavyotupa changamoto iliyojitokeza katika somo lililopita:-

 

Mfano 2:

<script>

   let a = 'mama anapika', b = 'ugalina dagaa';

   document.write(a, b);

</script>

code hizi zitakupa matokeo haya:-

Hapo utaona kuna changamoto kuwa variable ya kwanza na ya pili zimebanana. Hivyo unaweza kutengenisha nafasi hizi kwa kutumia html tag. Tunaweza kutatuwa changamoto hiyo kwa kutumia html tag <br> ila kwa kuwa hii ni string utahitajika kuiweka ndani ya zile alama za kufunga na kufunguwasemi yaani ‘<be>’

 

Mfano 3

<script>

   let a = 'mama anapika', b = 'ugalina dagaa';

   document.write(a, '<br>', b);

</script>

Hii itakupa matokeo haya

 

Hapo bado kuna changamoto kuwa badala ya maneno kuachana hapa yameachana na kuanza mstari mpya. Kwa kutima <br> utaanza msitari mpya kama inavyoonekana hapo. Ili kutatuwa hii unaweza kutumia alama zifuatazo 

 

 

  1. Kwa kutumia alama ya ku backlash ( )

Kwa kutumia alama hii utaweza kutenganisha nafasi kati ya variable mbili za string kama inavyoonekana kwenye mfano hapo chini:-

 

Mfano 3

<script>

   let a = 'mama anapika', b = 'ugalina dagaa';

   document.write(a, ' ', b);

</script>

 

Hii itakupa matokeo haya:-

 

Kufikia hapo tumeweza kutatuwa changamoto yetu.

 

Wacha nikupe changamoto nyingine. Angalia code hizi 

Mfano 4

<script>

  document.write("ng'ombe wababa")

</script>

Hizi zitakupa matokeo haya:-

Hapo neno ng’ombe limeandikika vyema kabisa. Ila changamoto ni kwenye code ghizi hapo chini 

 

Mfano 5

<script>

  document.write('ng'ombe wababa')

</script>

 

Code hizo hapo juu hazitakupa matokeo, kwa sababu zina error ni kwenye matumizi ya alama hii (‘). kwenye ng’o. Ili kutatuwa changamoto hii utatumia backlash yaani (). Hivyo code itatakiwa kuandikwa hivi:-

 

Mfano 6

<script>

  document.write('ng'ombe wababa')

</script>

Hii itakupa matokeo haya

 

Mwisho:

Tukutane somo la 6 tutakapokuja kujifunza jinsi ya kutumia matengo ya kihesabu kwenye javascript. Hapo utajifunza namna ya kupiga mahesabu kwa kutumia javascript na mengineyo zaidi.