Katika somo hili na linalofuata tutakwenda kutumia habari hii.

Umepewa kazi ya kuandika orodha ya maneno ya kiingereza na tafsiri yake kwa ajili ya kuandaa program ya kamusi. Sasa unatakiwa uonyeshe orodha ya maneno ambayo tayari umekusanya.

 

Angalia mfano hu:

Kwa kutumia safunzo yaliokwisha tangulia huko wali, nitaweka orodha ya maneno y bkiingereza kwenye array kisha nita display orodha hiyo kwa kuchanganya na maneno ya kiswahili. 


 

Sasa tuendelee na Somo letu. Hebu tuone jinsi ya kuonyesha orodha yetu kulingana na kile ambacho tulisha jifunza.

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  var words = ['mama - mother', 'dada - sister', 'kakav- brother', 'mjomb - uncle'];

  var show = "";

    show = show+ words[0]+'<br>';

    show = show+ words[1]+'<br>';

    show = show+ words[2]+'<br>';

    show = show+ words[3]+'<br>';

  

  document.write(show);

</script>

  </body>

</html>

 

Sasa hapo utaona tumerudia rudia statement moja ya ku display neno la kiingereza nankiswahili. Sasa kwa kutumia loop jatutakuwa tena na haja ya kurudia kuandika statement moja na badala yake tutaachia program irudie tena ku excute code.

 

Aina za loop

Kuan aina kuu 2 za loop ambazo ni 

  1. for loop
  2. for Of loop
  3. while loop

Poa kuna mgawanyiko zaidi tutakwenda kuuona tutakwpokuwa tunajifunza zaidi. Katika somo hili tutakwenda kujifunza luhusu for loop tu.

 

For loop;

Katika loop hii code zona excute kwa idadi maalumu unayoitaka. Kwa mfano list yetu hapo ina item 4, hivyo code zetu zita run mara 4. Unaweza kutumia 4 ama kutumia object length tulishasoma kwenye array jinsi ya kuoata array length. Hii itakupa idadi ya kuwa xode zitavexcute mara ngapi. Tunatumia hii ili kuhakikisha ina excute code kwa idadi maalumu ambayo inafanana sawasawa na item.

 

Lakini kama utaweka 4vits okey unaweza kuweka lia zaidi ya nne ama chini ya nne.

 

Kanuni ya kuandika for loop

Kwa nza utaanza na neno for likifuatiwa na mabano () ndni ha mabano kutakaa condition. Kisha itafuataiwa na na mabano {} ambapo ndani yake kutakaa statement ambayo itakuwa excuted kulingana na idani iliyowekwa.

 

Jinsi ya kuandika condition hapa kina utofauti mkubwa na tulivyojifunza huko awali. Katika for loop condition omegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni:-

  1. Initial expression yaani mwanzo wa loop. Hapa tutaangalia je loop yako unatakanianzie kwenye item ya ngapi. 
  2. condition Hapa sasa ndipo utaweka masharti yako, ambayo ikiwa yatafikiwa code zita excute na yasipofikiwa code zita stop
  3. Increment expression sehemu hii ndio ambayo inaangalia je code zinatakiwa kubexcuye mara ngapi. Lengo hili linafikiwa kwa kutumia increment (++)


 

Jambo la kuzingatia ni kutenganisha hizo sehemu tatu kwa nukta oacha semicolon ambazo ni (;). Kanuni hii itaandikwa hivi:-

for(initial expression; condition; increment){

statement

}

 

Katika initial expression utatumia variable kwa ajili ya kuhifadhi namba ambayo loop itaanzia. for(var i = 0;

 

Katika condition expression utatumia variable uliotengeneza pamoja na kuweka limit ya mara ngapi code zi excute. Unaweza kutumia i < 4; ama inaweza kuwa hivi i < array.length; neno array hapo nimelitumia kumaanisha object ya array.

 

Katika increment hapo tutatumia variable yetu inayobeba mwanzo wa loop kisha tutaiwekea increment (++). Mfano i++

 

Code nzima

for(var i =0; i<array.length; i++){

statement.

}

 

Angalia code hizi ambazo zinafanya kazi sawa na mfano wa hapo juu mwanzoni kabisa.

 

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  var words = ['mama - mother', 'dada - sister', 'kaka- brother', 'mjomb - uncle'];

  var show = "";

for(var i =0; i < words.length; i++) {

         show = show + words[i] + "<br>";

      }

    document.write(show);

</script>

  </body>

</html>

 

Sasa hapo utaona tumetumia array length kwa ajili ya kujuwa code zetu zita excute mara ngapi. Uzuri wa kutumia .length ni kwa kuwa hatujui code zetu zi excute mara ngapi. Ama tunatumia kwa ajili ya kuhakikisha kuwa item zote zitahusika kwenye excution ya code.

 

Sasa wacha tubadilishe. Sasa tunataka kwanza initial yetu ianzie na array ya 1 nancode zetu zi excute mara mbili 2. Mufanya hivi code zetu zitakuwa hivi

for(var i = 1; i < 2; i++)

 

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  var words = ['mama - mother', 'dada - sister', 'kaka- brother', 'mjomb - uncle'];

  var show = "";

for(var i =1; i <= 2; i++) {

         show = show + words[i] + "<br>";

      }

    document.write(show);

</script>

  </body>

</html>

 

 

Sasa endapo kwneye condition utaweka namba zaidi ya item code zitaendelea kufanya kazi ila zitaleta matokeo undefined kwa mfano tutaweka 8 hapo kwenye mfano wetu.

for(var i =0; i < 8; i++) hii itakuletea matokeo haya

Utaona hapo code zime excute mara 8 japokuwa item zilikwisha.

 

Break and continue

Sasa kuna jambo lingine. Chukulia mfano muwa unataka code zako zi excure mara mbili tu kisha zi stop.

Kufanya hivyo tutatumia break key word kama tulivyotumia kwenye switch. Hii tutaitumia ndani yastatemen yako.

 

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  var words = ['mama - mother', 'dada - sister', 'kaka- brother', 'mjomb - uncle'];

  var show = "";

for(var i =0; i < words.length; i++) {

  if(i ==2){

    break;}

         show = show + words[i] + "<br>";

      }

    document.write(show);

</script>

  </body>

</html>

 

 

Mfano meingine kwmba inataka loop yako istop inapofikia mara mbili kisha iruke moja halafu iendelee. Itaruka hapo ilipostop kisha inaendelea kubexcute. Kufanya hivi tutatumia continue yaani endelea. Kwa mfano una orodha ya watoto juma, hasaan, john, paul, rashid, daudi mwajuma sasa unataka kuita hii orodha kutoka juma ila unataka kumruka paul halafu unaendelea na rashidi. Hapa ndipo continue inapohitajika.

 

Kwanza kabisa itahitajika kumjuwa huyo tunayenruka ni array ya ngap. Kumbuka array huhisabiwa kuanzia 0. Hivyo paul ni array ya 3.

 

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  var watoto = ['juma', 'hassan', 'john', 'paul', 'rashidi', 'daudi', 'mwajuma'];

  var show = "";

for(var i =0; i < watoto.length; i++) {

  if(i ==3){

    continue;}

         show = show + watoto[i] + "<br>";

      }

    document.write(show);

</script>

  </body>

</html>

 

 

Utaona hapo paul hayupo kwenye orodha yetu. Hakuna kikomo vha ku break na ku continue. Unaweza ukawaruka zaidi na zaidi. Kwa mfano hapa chini tutakwenda kumruka rashidi array ya 4 na john array ya 2

<html>

  <head>

    <title>Mafunzo ya javascript</title>

  </head>

  <body>

<script>

  var watoto = ['juma', 'hassan', 'john', 'paul', 'rashidi', 'daudi', 'mwajuma'];

  var show = "";

for(var i =0; i < watoto.length; i++) {

  if(i ==2){

    continue;}

    if(i ==4){

    continue;}

         show = show + watoto[i] + "<br>";

      }

    document.write(show);

</script>

  </body>

</html>

 

 

Tikutane somo la 20 tutakwenda kujifunza kuhusu for of loop pamoja na while loop.