JINSI YA KUIFANYA BLOG IPATIKANE KWENYE SEARCH ENGINE KAMA GOOGLE
Search engine (Injini ya utafutaji ni nini?
Injini ya utaftaji ni mfumo wa programu ambao umeundwa kutekeleza utaftaji wa wavuti. Wanatafuta Wavuti Ulimwenguni kote kwa njia ya kimfumo kwa habari fulani iliyobainishwa katika swali la utaftaji wa maandishi. Wikipedia (Kiswahili)
Ni kazi yake Search engine yeyote iwe google ama nyingineyo kutafuta web ama blog yako popote ilipo. Ama kutafuta post ulioiandika popote pale ilipo. Hata hivyo hutokea kuwa ikashindwa kuona hiyo blog yako ama post yako. Hivyo utahitajika kuisaidia kujuwa namna ya kupata blog hiyo ama post yako. Zifuatazo ni njia za kuifanya blog yako ionekane kwenye search engine:-
1. Ruhusu blog yako ionekane kwenye search engine. Kwa wale wanaotumia blogger kuna mambo kadhaa unatakiwa uyafanye kwenye setting. Mambo hayo ni kama:-
- Ingi kwenye setting utaiona kwenye menu upande wa kushoto kisha kwenye kipengele cha Privacy kuna palipoandikwa Allow search engine to find your blog washa hicho kibatani.
- Kwenye hiyo setting shuka shini kuna palipoandikwa Crawler and indexing washa hicho kibatani kilichoandikwa Enable custon Robot.txt
Kwa wale ambao wanatumia wordpress ama website zao huna haja ya kufanya jambo lolote zaidi ya kusubiri hatuwa inayofuata. Kwa sasa hakikisha kuwa blog au website yako haihitaji password ili kuweza kuifikia. Ama kurasa ambazo unahitaji zionekane kwenye search engine hazihitaji mtu kulogin.
2. Isajili blog ama web yako kwenye search engine. Karibia search engine zote kubwa zina mfumo wa kuisajili website ama blog yako. Kwa mfano kwa google wanatumia Google Search Console kwa microsoft bing wanatumia Bing Webmaster Tools kwa yandex wanatumia Yandex Webmaster na zaidi ya hapo. Katika somo hili tutakwenda kuitumia google search console.
Unachotakiwa kufanya ni kujisajili kwenye hizo search engine kwa mfano Google search console Kwa kubofya link hii https://search.google.com/search-console. Utalog in kwa email yako, kisha Utatakiwa kuweka link au domain ya blog au website yako. Kule itaitwa property.
Kama hujanunua domain, weka link ya blog yako hapo palipoandika URL prefix. Kopi vyema link ya blog yako . Link utaipata kwenye upau wa juu wa kivinjari chako cha intanent. Angalia picha hii
Baada ya hapo, Pest hiyo link kwenye hicho kibox kilichoandika URL prefix. Itaonekana kama kwenye picha hapo chini
Hatuwa inayofauata bofya hapo palipoandikwa continue, itahitaji kufanya verification. Kwa wale wa blogger itajiverify yenyewe. Kama unatumia blog iliyo tofauti na blogger watakupa njia nyingine za kufanya verificationa kama kwa kutumia DNS kwenye domain, ama utapewa html code uziweke kwenye <head> ya blog ama website yako.
Pindi verifikation ikawa tayari bofya hapo palipoandika GO TO PROPERTY. Hpo moja kwa moja utapelekwa kwenye dashboard. Hapo utakuwa umeshaisajili web au blog yako kwenye search console ya google. Hivyo basi bofya START kuanza.
Kuna mambo mengi sana utatakiwa kuyajuwa hapo baadaye. Kwa sasa nitakueleza hili. Tunatakiwa tuongeze site map. Na utafanya hivi kila baada ya masiku kadhaa. Ijapokuw ahili sio la lazima kwani google wenyewe wanaitafuta blog iliyopo kwenye blogger. Lakini utahitajika kufanya hivi mara kwa mara kama unatumia website hasa zile za html.
Kwenye dashoard kuna palipoandika SITEMAPS. Kikawaida search engine huhitaji sitemap ili kuweza kuziona post au makala zote zilizomo kwenye blog ama tovuti husika. Kwa wale wa blogger utainia hapo site map kisha
Kisha kitakuja kijibox ambapo utatakiwa kuweka link ya sitemap. Wale wa blogger hapo weka sitemap.xml kama inavyoonekana kweye picha hapo chini. Na wale wanaotumia website za html, au wordpress ama blog nyinginezo utahitajikakutengeneza sitemap yako kisha unakuja ku pest link hapo.
Kutengeneza sitemap utahitajika kufuata maelekezo vyema ama tumia website hii http://www.check-domains.com/sitemap/index.php hapo utatengeneza site map, kisha uta iupload kwenye web yako. Kisha utachukuw alink na kuja kuipest hapo. Ukimaliza bofya submit. Kama imekubaliwa utapokea ujumbe huu
Vinginevyo utarudia. Lamda tu nikujuze kuwa sitemap inakuwa na orodha ya post zote, au makala zote. Hivyo maroboti ya search engine watatumia hiyo kama kielekezi cha kuangalia post ambayo haipo kule ama imefanyiwa marekebisho na kuiupdate kwenye search engine.
Kila utakapoona kuna post au makala mpya na haipatikani kwenye search engine ni vyema utengeneze site mapa ambayo itakuwa na link ya hiyo post au makala mpya.
Mpaka kufikia hapa utakuwa umesha ifanya blog ama web yako ipatikane kwenye Google search engine.
3. Shea blog ama web yako zaidi na zaidi.
Kama nilivyokueleza kuwa search engine zitaitafuta web/blog yako popote pale ilipo. Hivyo kila ukishea ndipo unawarahisishia hawa maroboti quinoa hiyo post au maka. Unaweza kutumia facebook, youtube comment box, blog comment box na social media nyingine.
4. Hakikisha blog ama web yako ni salama. Search engine wataikataa link yeyote ile ambayo haipo salama. Na wanaweza pia kuifunga web ama blog yako.
5. Andika maudhui nzuri, wacha kukopi na kupest mitandaoni. Tumia lugjha nzuri. Pia hakikisha hiyo blog ama tovuti ni rahisi kuitumia. Pia kurasa zote unazotaka zionekane kwenye search engine hazihitaji kujisajili.
Mwisho:
Kwatika somo linalofuata tutakwenda kujifunza jinsi ya kubadilisha template ya blog ili kuboresha muonekano