JINSI YA KUTENGENEZA BLOG KWA KUTUMIA BLOGGER:
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kutengeneza blog yako mwenyewe kwa kutumia mtandao wa blogger. Haya ni maelekezo mafupi ambayo yanatumia dakika zisizozidi 10 mpaka kukamilisha kuwa na blog yako.
Vigezo:
- Uwe na email ya gmail
- Uwe na simu ama kompyuta
- Juwe kusoma na kuandika
Kama upo tayari kuanza kufunguwa blog yako. Fuata maelekezo yafuatayo.
- Kingia kwenye tovuti hii blogger.com
Kama huja log in upande wa kulia wa ukurasa huu kwa juu kuna sehemu imeandikwa sign in utabofya hapo ili kulogin kwa email ya gmail. Kwa juu katikati chuka chini kidogo kuna batani imeandikwa create your blog bofya hapo. Angalia picha hapo chini. Kama hujalogin utaendelea ku login ama kama tayai utapelekwa ukurasa mwingine.
- Baada ya hapo ukurasa utakaofunguka utakuhitaji kuweka jina la blog kwenye Title jina lisizidi herufi 100. Ni vyema jina likawa fupi na lenye kueleweka vyema. Kwa mfgano tutakwenda kutengeneza blog yetu yenye jina la tehama. Hivyo kwenye Title nitaweka Tehama. Kisha baada ya kuandika jina la blog utabofya next chini upande wa kushoto. Angalia picha hapo chini.
Baada ya hapo ukurasa mwingine utafunguka. Huo utakuhitaji kuweka anuani ya blog yaani address ama url. Hii ni link ambayo blog yako itapatikana. Hapo utajaribu maneno kadhaa ambayo yanaendana na jina la blog yako. Kama hamuna blog ambayo ina url sawa na hiyo unayoweka itakubaliwa, ila kama imeshatumika itakataliwa.
Anjani yako ifuate sheria hizi:-
- Usiache nafasi kati ya neno na neno
- Usitumie special character kama @, %, #, na nyinginezo kama mabano
- Vyema usitumie namba tupu ambasuchanganye namba na herufi
- Vyema isiwe ndefu
- Usichanganye herufi ndogo na luwa
- Anuani iwe rahisi na yenye kueleweka.
Kama nilivyokueleza awaku, hapo unaweza kuweka maneno kadhaa yakakataliwa. Wacha tuweke tehama uone kama litakubaliwa.
Utaona hapo tumeambiwa address is not available yaani hiyo anuani tayari imeshatumiwa. Hivyo tutajaribu ningine. Utaona hapo mbele kuna neno blogspot.com hii ni domain ambapo blog yako itakaa. Utakapotaka kuondosha hayo mabneno utatakiw akununua jina yaani domain. Nitakufynsiha mbeleni.
Sasa nakwenda kuweka neno tehamatzbongo. Utaona hapo chenye picha nimembiwa this address is available maana yake anuani hii ipo. Hivyo blog yetu itaipatikana kwa link hii tehamatzbongo.blogspot.com kwa wewe u=utatafuta neno ambalo litakuwa tayari. Baada ya hapo utabofya next kwa chini upande wa kushoto.
Ukurasa utakaofuata utakuhitaji kuweka jina ambalo litakuwa likionekana kwenye blog yako. Unaweza kuweka jina lolote ila lisizidi herufi 200. Hapa sitokwenda mbali sana na jina tuliloweka mwanzo. Hapa nakwend akueka Mafunzo ya Tehama. Baada ya hapo bofya neno finish kwa chini upande wa kulia.
Mpaka kufikia hapo blog yetu imekamolika. Kutaka kuiona blog yetu bofya hapo palipoandikwa view blog chini kapisha nimeweka namba 2 . Utaona kajiblog ketu hapo tayari. Ila sasa haina post hata moja. Somo linalofuata litakwenda kukufundisha jinsi ya kuandika post. Blog yetu tulioitengeneza utaipata hapa https://tehamatzbongo.blogspot.com/
Mwisho:
Katika somo linalofuata utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika post yako ya kwanza. Ama unaweza kufanyia mazoezi hapo nilipoweka nmaba 1 kwenye picha hapo juu.