Kama unatumia simu upande wa kushoto kuna menu hapo bofya utaletewa list ya menu. Bofya palipoandikwa NEW POST. na kama unatumia kompyuta bofya palipoandikwa NEW POST upande wa kushoto kwa juu.
Kama unatumia simu ukurasa utakaofunguka utakuwa tofauti na wanaotumia kompyuta. Hata hivyo nitafafanua kwa manufaa ya wote wanaotumia simu na kompyuta. Hapo chini naleta picha mbili moja kwa wanotumia simu na ingine ni kwa wanaotumia kompyuta.
Kwa watumiaji simu
Kwa watumiaji kompyuta
- Hapo kwenye namba 1 ndipo utakwenda kuandika kichwa cha habari cha hiyo post yako.
- Kwenye namba 2 ni kwa ajili ya ku preview yaa ni kuangalia jinsi ambavyo post yako itaonekana na wasomaji wako kabla hujaipost
- Kwenye namba 3 hapo ndipo utakapobofya pindi unapomaliza. Ukibofya hapo post yako inakuwa live. Hivyo watu wote wataweza kuiona.
- Hiyo ni menu ambapo kila unachokiona hapo kitakusaidia katika kuboresha muonekano wa post. Kwa wanaotumia siku buruza huo mstari utakuonyesha menu zaidi.
- Kwenye nmaba 4 hapo hutumika ku edit html code za hiyo post yako. Kama unataka kuongeza maboresho kwa kuweka code za html, css na javascript kwenye post yako, basi hapo ndio sehemu inayotumika.
Menu ya vifaa vya uandishi
Sasa ngoja tuone baadhi ya sehemu muhimu katika uandishi wa post yako kwenye blog.
- Ni kwa ajii ya kufanya herufi kuwa bold
- Ni kwa ajili ya kufanya maandishi kuwa italics
- Ni kwa ajili ya kupigia mstari maandishi
- Kwa ajili ya kukata maadhishi
- Kwa ajili ya kuweka rangi kwenye maandishi
- Kwa ajili ya kuweka rangi ya background
- Kwa ajili ya kuweka link
- Kwa jili ya kuweka picha
- Kwa ajili ya kuweka video na audio
- Kwa ajili ya kuweka emoj
- Kwa ajili ya kupangilia muonekano wa paragraph
- Kwa ajili ya kupangilia mtiririko wa namba
- Kwa ajili ya kunukuu
Mfano wa post
Ni nini maana ya blog
Neno "blog" linatokana na neno la Kiingereza "weblog," ambalo ni kifupi cha maneno "web" na "log." Katika Kiswahili, "blog" inaweza kutafsiriwa kama "blogu."
Blogu ni aina ya tovuti au ukurasa wa mtandao ambapo mtu au kikundi cha watu hutoa maudhui yanayopangwa kwa utaratibu wa wakati, na mara nyingi maudhui hayo yanahusu mambo ya kibinafsi, uzoefu, maarifa, au mada nyingine zinazovutia mwandishi wa blogu au wasomaji wake.
Mwandishi wa blogu hujulikana kama "blogger," na anaweza kuchapisha machapisho (posts) mapya mara kwa mara. Hii inaweza kujumuisha maandishi, picha, video, au hata sauti. Watu hupenda kufanya blogu kama njia ya kushiriki uzoefu wao, mawazo, au maarifa na wengine kwenye mtandao.
Blogu zinaweza kuwa za aina nyingi, kama vile blogu za kibinafsi, blogu za habari, blogu za mada maalum, na kadhalika. Ni jukwaa lenye mwingiliano na huruhusu watu kutoa maoni na kushirikiana na mwandishi na wasomaji wengine.
Weka post hiyo ukimaliza weka na picha, baada ya hapo bofya batani ya ku publish rejea picha hapo juu namba 3. Ukisha bofya utarudishwa kwenye dashboard. Dashboard hiyo itakuletea vitu vingine vipya.
Kwa watumiaji wa simu:
Kwa watumiaji wa kompyuta:
- Hiyo ndio menu ambapo watumiaji wa simu atabofya ili kupata menu kuu
- Hapo panaonesha tarehe ambayo post iliandikwa. Pia kwa watumiaji wa kompyuta ukiweka cursor hapo ndpo utapata menu kuu hiyo. Kazi nyingine ya hapo ni kuwa ukibofya utakwenda ku edit post. Hivyo kama unataka kuifanyia mabadiliko bofya hapo
- Ni kwa ajili ya kufuta post.
- Kwa ajili ya kuweka lebel
- Kama hutaki post iwe live kwenye blog utabofya hapo, post itakuwa ni draft
- Hiyo ni kwa ajili ya kuangalia post yako live.
Pia kuna menu nyingine ndogo chini ha hiyo menu kuu, angalia picha hapo chini:
- Hiyo ni kwa ajili ya ku share post yako
- Hiyo inaonyesha idadi ya comment kwenye hiyo post
- Hiyo ni kuangalia comment
- Inaonyesha idadi ya watu walioisoma
- Ni kwa ajili ya kuagalia takwimu zinazohusu hiyo post
Mwisho:
Tukutane somo linalofuata tutakwend akujifunza jinsi ya kuifanya blog yako ionekane Google.