Somo la 4 Python sqlite: Jinsi ya kuingiza data kwenye table na database

INSERT ndio roho ya kuanza kujaza database na kufanya iwe na maana. Tumeunda kabati la faili (database) na droo (meza), sasa ni wakati wa kuweka taarifa zetu za kwanza.

 


 

Kuelewa Syntax: INSERT INTO

 

Amri ya INSERT INTO ndio tunayotumia kuongeza mstari mpya (record) kwenye meza yetu. Muundo wake wa jumla unaonekana hivi:

INSERT INTO jina_la_meza (safu1, safu2, ...) VALUES (thamani1, thamani2, ...);

Katika Python na SQLite, hatutumii amri hii moja kwa moja. Badala yake, tunatumia placeholders (?) ili kuzuia mashambulizi ya kiusalama yanayojulikana kama SQL Injection. Njia hii ni salama zaidi na inafaa zaidi kwa programu.

Unda faili jipya liite insert.py kisha paste code hizi. 

NB: Ni vizuri kuandika mwenyewe ili kupata uzoefu thabiti.

import db_conn as dbConn

def InsertData(name:str, takenBy:str, quantity:int, location:str, price:int):
    connection = dbConn.get_connection()
    pointer = connection.cursor()
    query = """
    INSERT INTO products (name, taken_by, quantity, location, price) VALUES (?, ?, ?, ?, ?)
    """
    data = (name, takenBy, quantity, location, price)
    pointer.execute(query, data)
    connection.commit()
    connection.close()
    print('Taafifa zimeifadhiwa kikamilifu')
   
   
def getUserData():
    try:
         Name = input('Ingiza jina la bidhaa > ')
         TakenBy = input('Jina la mdeni > ')
         Quantity = int(input('Kiasi cha bidhaa > '))
         Location = input('Eneo la mdeni > ')
         Price = int(input('Bei ya bidhaa > '))
         
         InsertData(Name, TakenBy, Quantity, Location, Price)
         
    except ValueError as error:
        print(f'Kosa: {error}')

getUserData()
 

Kuvunja Msimbo na kuelewa Kila Kazi

 

Hebu tuchambue code ili kuelewa kila sehemu.

 

1. Kazi ya InsertData()

 

Kazi hii inachukua data kutoka kwa mtumiaji na kuihifadhi kwenye database.

 

2. Kazi ya getUserData()

 

Kazi hii inasimamia mchakato wa kupokea data kutoka kwa mtumiaji.

 

Mambo ya msingi kufahamu

Unapaswa kuelewa kwamba kuna hatua tatu muhimu za kufanya kazi na database:

  1. Muunganiko na Cursor: Kwanza, unahitaji kuunganisha na database na kupata cursor.

  2. Kutekeleza Amri: Pili, unatumia cursor kutekeleza amri za SQL kama INSERT.

  3. Kuhifadhi Mabadiliko: Mwisho, unatumia commit() kuhifadhi mabadiliko na close() kufunga muunganiko.

VIDEO TUTORIALl: ?

Tazama au Download video hapa

MWISHO:

Katika somo linalofuata tutajifunza namna ya kusoma data kutoka kwenye database yetu