Somo la 2 Python Sqlite na muunganiko wa Database (Database Connection)

 

Muunganiko (connection) wa database ni daraja au njia ya mawasiliano kati ya programu yako ya Python na database yenyewe. Ili programu yako iweze kusoma, kuandika, au kufanya mabadiliko yoyote kwenye data iliyohifadhiwa, lazima kwanza iunganishe na database.

Kwa nini ni muhimu?

 


 

2. sqlite3.connect() - Jinsi Daraja Linavyojengwa

 

Kazi (function) ya sqlite3.connect() ndiyo inayojenga daraja hili.

 


 

3. conn.cursor() - Mtendaji wa Kazi

 

Baada ya kuwa na muunganiko (connection), unahitaji mtu wa kutekeleza amri zako za SQL. Huyu ndiye cursor.

 


 

4. Mzunguko wa Muunganiko (Connection Lifecycle)

 

Kuna hatua tatu muhimu za kuzingatia kila unapofanya kazi na database:

  1. Muunganiko (Connection): Anza kwa kuunganisha na database kwa kutumia sqlite3.connect().

  2. Kutekeleza Amri (Execution): Tumia cursor kutekeleza amri za SQL.

  3. Kufunga (Closing): Funga muunganiko kwa kutumia conn.close() baada ya kumaliza kazi. Hii ni muhimu kwa usalama na utendaji. Inahakikisha kwamba rasilimali zilizotumiwa zinarudishwa na kwamba mabadiliko yote yamewekwa vizuri.



Mfano wa kuunganisha database.

import sqlite3

 

def GetConnection():

    # Tunatumia 'try' kuanza kizuizi cha msimbo unaoweza kuwa na shida

    conn = None

    try:

        conn = sqlite3.connect('business.db')

        print("Muunganiko na database umefanikiwa.")

        return conn

    except Exception as e:

        # 'except' inakimbilia hapa kama kuna shida ya muunganiko

        print(f"Tatizo la muunganiko: {e}")

        return None

    finally:

        # 'finally' inahakikisha msimbo huu unafanya kazi kila mara.

        # Tunafunga muunganiko hapa kwa usalama, ingawa unaweza kuufunga

        # baadaye baada ya kumaliza shughuli.

        if conn:

            conn.close()

            print("Muunganiko umefungwa.")

 

#Tunaita function ya connection

GetConnection():

 

Uki run script hii utaona file jipya limeundwa ndani ya root folda yako. Kwa kawaida file hili linapoundwa (business.db) Linakuwa empty yaani tupu kwani hatujaunda hata table moja ndani yake.

VIDEO TUTORIAL ?:

Tazama na download video hapa

 

Mwisho:

Katika somo litakalofuata tutaenda kujifunza jinsi ya kuunda table kwenye database yetu ya business.db