OOP ni kifurushi Cha maneno Object Oriented Programming. Huu ni mtindo wa ku code kwa kukusanywa function zote zinazofanana kwenye ukurasa Moja unaoitwa class Ili kueepuka Hali ya kurudis rudia code katika program.

 

Ili kuelewa vyema ni Nini OOP Wacha kwanza nikufundishe kuhusu programming paradigms.

 

Je ni Nini programming paradigms?

Hizi ni staili ama mitindo ambayo hutumika na ma programmer katika uandishi wa program. Kila staili ila faida na hasara zake, ia Kila Moja Ina maeneo ambayo inafaa zaidi kutumiwa.

 

Kuna paradigms zisizopinguwa nne ambazo ni:-

  1. Imperative programming
  2. Declarative programming
  3. Procedural programming
  4. Functional programming
  5. Object oriented


 

Faida kubwa ya kutumia OOP ni kufanya code zako ziwe DRY yaani Don't Repeat Yourself.

 

OOP ilianza kwenye PHP toleo la 5. Ina maana kabla ya hapo PHP ilitumia procedural programming tu. Baada ya kuonekana umuhimu wa OOP kama ilivyokuwa ikitukiwa na language zinginezo wakati huo.

 

Faida za OOP

  1. Ipo faster zaidi kuliko procedural
  2. Ni rahisi kuitumia zaidi na zaidi
  3. Ipo salama zaidi kuliko procedural
  4. Code zako zinakaa vyema zaidi yaani clean

 

Zingatia:-

Tumia procedural ikiwa project ni ndogo na huna ulazima wa kutumia code hizo muda mwingine.

 

Kama project ni kubwa tumia OOP ama kama unahitaji kutumia tena hizo code tumia OOP.

 

Hakikisha una uelewa na procedural programming kabla ya kuanza kujifunza OOP.

 

Mambo muhimu kwenye OOP

OOP imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo ni class na object

 

Class na object

Ili uweze kujuwa class na object tofauti zao angalia mfano huu. Chukulia gari aina ya Toyota. Sasa hapa tunasema gari ni class na Toyota ni object. 

 

Kwahiyo tunaweza sema kwamba gari ikawa katika aina mbali mbali kama Toyota, scania, BMW. Kila gari katika hizo ikawa na sifa zake kama rangi, speed, transition. Na ikawa rangi ni buluu, speed 180km/h, transition automatic. Sasa hapo tunasema:

Class ni gari

Object ni toyota

Property ni rangi, speed, transition

Value ni buluu, 180km/h, automatic

 

Class ndio hubeba hizo property na object hubeba hizo values. Hivyo Kila kunapokuwa na objects inarithi property zote.

 

Ndio maana tunasema class ni template ya object.


 

Mambo ya kuzingatia

Kwenye class variable huitwa property na function huitwa method.