Matumizi ya __construct() function kwenye class.

Hii hutumika Ili kuweza kuanzisha (iniate) object mara TU baada ya kutengeneza. Kuanzisha object ni kule kuipa thamani value yake. Kama tulivyoona huko mwanzoni baada ya kutengeneza object Kisha tukaioa thamani yake.

 

Tunatumia alama mbili za underscore yaani (_ _).

 

Sasa unapotumia __construct() function basi value ya object utaweka Moja kwa itMoja pinde TU unapotengeneza object.

Mfano:

<?php

class gari{

public $name;

 

function __construct($name){

$this->name = $name;

}

 

function get_name(){

return $this->name;

}

 

}

//tengeneza object

$jina = new gari("toyota");

echo $jina->get_name();

 

?>

 

Ukiangalia vyema __construct() inasaidia sana katika kupunguza kazi.  Maana unaweka value moja kwa moja unapotengeneza object. 


 

Matumizi ya __destruction function

Wakati construct hutumika wakati wa kutengeneza object, hii ya distruct hutumika wakati program inapostop, Ina maana distruct function itafanyabkwzi mwishoni mwa program.

 

<?php

class gari {

  public $jina;

  public $speed;

 

  function __construct($jina) {

    $this->jina = $jina;

  }

  function __destruct() {

    echo "Jina la gari ni {$this->jina}.";

  }

}

$toyota = new gari("Toyota");

 

echo "Lina rangi ya njano";

echo "<br>";echo "<br>";

?>

Hapo ilitakiwa ianzie jina la gari ni Toyota Kisha ndipo ifuatie Lina rangi ya njano . Ila kwa kuwa tumetumia destruct yenyewe itafanya kazi mwishoni mwa program.