Cookie Headers
HTTP cookie ni kifaili kidogo chenye data ambacho huhifadhiwa kwenye browser ya mtumiaji. Cookie hutumika kwa kazi nyingi kama kufanya session, kufuatilia mtumiaji ama kutumia taarifa za mtumiaji ili kuboresha matumizi yake.
Kuna http header mbili ambazo zinahusiana na cookie ambazo ni:-
-
Set-Cookie Header
-
Cookie Header
Set-Cookie Header
Hii hutumika na server kutuma taarifa kwenye browser ya mtumiajiili k set cookie mpya yaani kutengeneza cookie.
Jinsi ya kutengeneza cookie
Ili kutengeneza cookie tutatumia function ya setcookie() ambapo itakuwa na jina la cookie - name kisha thamani ya cookie - value na itafuatiwa na attribute za cookie ambazo ni:-
-
Expire hii huonyesha ni baada ya muda gani cookie zita expire huandikwa kwa sekunde
-
Path hii hueleza sehemu ambapo itatumika kama ni website yote utaweka slash (/) ama kamaunataka kwa baadhi tu ya mafolder utaweka location ya folder
-
Domain: hapa utataja domain ambayo hiyo cookie itatumia. Hii ni kwa aili ya usalama zaidi.
-
Secure hapa ni kwa ajili ya kuonyesha je unataka cookie zitumike kataika https - kwa usalama zaidi ama kwa http utaweka true kama ni https
-
Httponly hii hueleza header ni protocol gani itatumia hizo cookie. Protocal zipo nyingi kama http, ftp, smtp, tcl n.k. Sasa ukiweka true maana yake itatumika kwenye http tu.
Mfano:
<?php
setcookie('user','Bongoclass',time()-3600,'/','bongoclass.com',true,true);
echo $_COOKIE['user'];
Ikitokea unataka kufuta cookie utaset time negative. Badaa ya kuweka time() +600 utaweka time() - 3600 ama namba yeyote iliyo negative.