STATIC METHOD
Hii ni method ambayo inaweza kutumika moja kwa moja bila ya kutengeneza class instance (yaani bila ya kutengeneza object). Kutengeneza static method tutatumia keyword static . angalia mifano hapo chini kwanza nitakuletea mfano wa function ambayo sio static. Na kisha ambayo ni static.
Mfano1;
<?php
class gari {
public function tangazo() {
echo "Tunauza gari";
}
}
$my = new gari();
$my->tangazo();
?>
Utaona hapo ili tuweze kuitumia method tangazo imetubidi kwanza kutengeneza instance of class hapo tumeanza kwanza kutengeneza object $my = new gari(); Wacha sasa tuone mfano wa method hii hii ila ikiwa static utaona hapo hatuna haja ya kutengeneza object tena yaani instance of class. Pia tutatumia scope operator (::)
<?php
class gari {
public static function tangazo() {
echo "Tunauza Gari";
}
}
gari::tangazo();
?>
Pia endapo ststic method itatumika ndani ya class tutatumia keyword self ikifuatiwa na scope operator (::)
<?php
class gari {
public static function tangazo() {
echo "Tunauza magari";
}
public function __construct() {
self::tangazo();
}
}
new gari();
?>
Pia static method inaweza kutumiwa na class nyinginezo. Ila sharti iwe ni public method
<?php
class gari {
public static function tangazo() {
echo "Tunauza gari";
}
}
class toyota {
public function ujumbe() {
return gari::tangazo(). " aina ya toyota";
}
}
$obj = new toyota();
echo $obj -> ujumbe();
?>
Sasa ikiwa unataka kutumia static method kwenye child class hapo tutatumia keyword parent angalia mfano hapo chini.
<?php
class gari {
protected static function tangazo() {
return "Tunauza gari";
}
}
class toyota extends gari {
public $jina;
public function __construct() {
$this->jina = parent::tangazo(). " aina ya toyota";
}
}
$myob = new toyota();
echo $myob -> jina;
?>
Mwisho
Katika somolinalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu static property