kwa kutumia IP address kuna taarifa nyingi za mtumiaji unaweza kuzipata kama vile:-
- mahala alipo
- mtandao wa skimu anaotumia
- code ya nchi
Na nyinginezo nyingi. katia somo hili tutatumia free API za iplocation.net. Kmbuka kuwa endapo mtu atatumia VPN taarifa utakazopata hazitakuwa sahihi kwani VPN inaficha IP address halisi ya mtumiaji.
Kwa kutumia hii API utaweza kupata jina la nchi kwa kutumia country_name, code ya nchi kwa kutumia country_code2, mtandao wa internet ama ISP kw akutumia isp. Angalia mfano wa code hizo hapo chini:-
<?php
$userIp = $_SERVER['REMOTE_ADDR'];
$ipLocationObj = json_decode(file_get_contents(
"https://api.iplocation.net/?ip={$userIp}"
));
$country = $ipLocationObj->country_name ?? "";
echo $country;
echo '<br>';
$isp = $ipLocationObj->isp ?? "";
echo $isp;
echo '<br>';
$code = $ipLocationObj->country_code2 ?? "";
echo $code;
Mfano wa matokeo kwa IP ya Tanzania
Tanzania, United Republic of
MIC Tanzania Ltd
TZ