Sheria za Kuandika JSON
Kabla ya kuanza kuandika JSON, ni muhimu kuelewa sheria zake. Sheria hizi zitakusaidia kuandika data sahihi na kuepuka makosa.
1. JSON Huandikwa kwa Jozi za Key na Value
-
Kila jozi ya data ina key na value.
-
Key ni jina la data na value ni thamani ya data hiyo.
-
Kati ya key na value, tumia alama ya nukta mbili (:).
Mfano:
"jina": "John Doe"
2. Key Lazima Ziwe Ndani ya Alama za Semi Mbili ("")
-
Key zote lazima ziwe ndani ya alama za funga semi mbili.
-
Thamani (value) ya aina ya maandishi (string) pia huwekwa ndani ya alama za semi mbili.
Mfano:
"jina": "John Doe",
"mji": "Mpanda"
3. JSON Huandikwa Ndani ya Mabano Makubwa ({})
-
Data yote ya JSON lazima ianze na kifungua bano kubwa { na kumalizika na kifunga bano kubwa }.
Mfano:
{
"jina": "John",
"umri": 30
}
4. Value Zinaweza Kuwa Aina Mbalimbali za Data
-
Aina za data zinazokubalika kwenye JSON ni:
-
String: Maandishi, huwekwa kwenye alama za semi mbili ("example").
-
Number: Namba kamili au zenye desimali (30, 12.5).
-
Boolean: Thamani za true au false.
-
Null: Thamani isiyo na kitu (null).
-
Array: Orodha ya thamani nyingi, huwekwa kwenye mabano ya mraba ([]).
-
Object: JSON ndani ya JSON, huwekwa kwenye mabano makubwa ({}).
Mfano:
{
"jina": "John Doe",
"umri": 30,
"ndoa": true,
"simu": null,
"watoto": ["Anna", "Ella"],
"anwani": {
"mtaa": "Kigonzi",
"mji": "Mpanda"
}
}
5. Data Katika Array Huandikwa Ndani ya Mabano ya Mraba ([])
-
Orodha ya thamani nyingi huandikwa kwenye mabano ya mraba na kutenganishwa kwa koma.
Mfano:
"masomo": ["Hisabati", "Sayansi", "Historia"]
6. Data Lazima Itenganishwe na Koma (,)
-
Kila jozi ya key na value lazima itenganishwe na alama ya koma, isipokuwa jozi ya mwisho.
Mfano:
{
"jina": "John Doe",
"umri": 30,
"ndoa": true
}
7. Hakikisha Ulinganifu wa Mabano
-
Mabano yote yaliyofunguliwa lazima yafungwe.
-
Usahihi wa mabano ni muhimu ili JSON isomwe bila makosa.
Mfano Sahihi:
{
"jina": "John",
"watoto": ["Anna", "Ella"]
}
Mfano Usio Sahihi:
{
"jina": "John",
"watoto": ["Anna", "Ella"
8. Hakuna Alama za Ziada Mwisho wa JSON
-
JSON isimalizike kwa alama ya koma au neno lolote lisilohitajika.
Mfano Sahihi:
{
"jina": "John",
"umri": 30
}
Mfano Usio Sahihi:
{
"jina": "John",
"umri": 30,
}