Aina za Data Zinazotumika kwenye JSON

JSON inasaidia aina chache za data, lakini ni za msingi na zinalingana na aina nyingi za data katika lugha za programu. Hapa kuna orodha ya aina za data zinazotumika kwenye JSON pamoja na mifano ya jinsi zinavyoandikwa:

 


 

1. String

Ni mfululizo wa herufi zilizoandikwa ndani ya alama za nukuu mbili (" ").

Mfano:

{

  "jina": "Amina",

  "nchi": "Tanzania"

}

Hapa, jina na nchi ni keys, na "Amina" na "Tanzania" ni strings.

 


 

2. Nambari (Number)

Inajumuisha namba za kawaida (nzima au desimali). JSON haina tofauti kati ya namba nzima (integer) na desimali (float).

Mfano:
{

  "umri": 25,

  "kiwango": 95.6

}

umri ni namba nzima (integer), na kiwango ni namba ya desimali (float).

 


 

3. Boolean

Ni thamani ya kweli (true) au si kweli (false).

Mfano:
{

  "ndoa": true,

  "elimu_imekamilika": false

}

ndoa inaonyesha kweli (true), na elimu_imekamilika inaonyesha si kweli (false).

 


 

4. Null

Inawakilisha thamani isiyo na kitu au hakuna thamani.

Mfano:
{

  "jina_la_pili": null

}

jina_la_pili halina thamani, hivyo linawekewa null.

 


 

5. Orodha (Array)

Ni mkusanyiko wa thamani nyingi zilizoandikwa ndani ya mabano ya mraba ([ ]). Thamani zinaweza kuwa za aina yoyote inayokubalika katika JSON.

Mfano:
{

  "watoto": ["Anna", "Ella", "Sam"],

  "alama": [85, 90, 78.5]

}

watoto ni orodha ya strings.

alama ni orodha ya namba (nzima na desimali).

 


 

6. Vitu (Object)

Ni mkusanyiko wa key-value pairs zilizoandikwa ndani ya mabano ya mkunjo ({ }).

Mfano:

{

  "anwani": {

    "mtaa": "Kigonzi",

    "mji": "Mpanda",

    "postikodi": 50100

  }

}

anwani ni kitu ambacho kina key-value pairs tatu (mtaa, mji, postikodi).

 


 

7. Nested Objects

Hii ni hali ambapo vitu (objects) vinaweza kuingizwa ndani ya vitu vingine au orodha.

Mfano:
{

  "mwanafunzi": {

    "jina": "Amina",

    "umri": 25,

    "alama": {

      "hisabati": 85,

      "sayansi": 90

    },

    "vitabu": ["Fizikia", "Kemia", "Biolojia"]

  }

}

mwanafunzi ni kitu chenye keys jina, umri, alama (ambacho ni kitu kingine), na vitabu (ambayo ni orodha).