OOP ni kifupisho cha maneno Object Oriented Programming. Hii ni moja katika mitindo inayotumiwa kwenye programming yaani (programming paradigm) mitindo mingine ni kama 

  1. Imperative programming
  2. Declarative programming
  3. Procedural programming
  4. Functional programming

Dart ni Object Oriented Programming language kwa maana kila kitu kinachukuliwa kama object kwenye Dart. Kwenye OOP object inaweza kuwa kitu chochote kama gari, mbuzi, kondoo, simu. Kisha object inakuwa na sifa zake kama vile urefu, rangi, kimo, ukubwa. Pia object inakuwa na tabia kama kutembea, kuzungumza, kucheka, kuharibuka. Hizi sifa huitwa attributes na hizi tabia huitwa behaviour

Faida za OOP

  1. Ni rahisi kuelewa code zake na kuzitumia
  2. Ni rahisi kutumia code zaidi na zaidi kwa urahisi.
  3. Inakuwa rahisi kukamilisha program
  4. Ni rahisi kwa ajili ya team work yaani katika kushirikiana.
  5. Husaidia kupunguza hali ya kurudia rudia kuandika code.

 

Features za OOP:

Ii ni misingi ya OOP. utakapokuwa umeelewa misingi hii basi itakuwa rahisi kutengeneza program kwa OOP:

  1. CLASS
  2. OBJECT
  3. ENCAPSULATION
  4. INHERITANCE
  5. POLYMORPHISM
  6. ABSTRACTION

 

Kuna baadhi ya misamiati unaweza kukutana nayo kwenye OOB kama method na properties. Methods hizi ni function na properties ni variable. Nimerahisisha hivi ili update kuelewa vyema inaposemwa property nini hasa kinaweza kumaanishwa.

 

Mwisho:

Somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu class na jinsi ya kuitengeneza.