While loop hii hutumika endapo hujui kama code zako zinatakiw aku run mara ngapi. Yenyewe hii ni rahisi sana kutumia. Unachotakiwa kufanya ni kuweka sharti (condition) kisha zitafuata code.

While (condition){

Code

increment/ decrement

}

void main() {

 print('ORODHA YA NAMBA');

 var x = 1;

 print(x);

 while(x <12){

   x++;

   print(x);

 }

}

 

 

Wach tuone jinsi ambavyo tutaweza kutengeneza tebo yetu ya 7 kwa kutumia while loop.

 

void main() {

 print('TEBO YA 7');

 var x = 0;

 while(x <12){

   x++;

   print("${x}*7= ${x *7}");

 }

}

 

Do while loop

Hii ni sawa na while loop ila utofauti wao ni kuwa do while loop yenyewe kwanza itanza na ku run code husika kabla ya kuangalia sharti. Baad ya ku run mara moja ndipo inaangalia sharti zilizowekwa, kama zitatimia itaendelea ku run ila zisipotimia itastop.

 

Kanuni yake:

do {  

code

}while(condition);  

 

void main() {

 var x = 1;

 print('TEBO YA 7');

 do{

   print("${x}*7= ${x *7}");

   x++;

 }while(x<=12);

}

 

Ukiangaia vyemahapo kwanza tumianza ku print print("${x}*7= ${x *7}");

Kisha ndipo tukafanya increment. Na baadaye tuakaangalia sharti kama zimefikiwa. Sasa ngoja tubadili shari tuone, tunabadili badala ya x<=12 tunakwenda kuweka x>12

void main() {

 var x = 1;

 print('TEBO YA 7');

 do{

   print("${x}*7= ${x *7}");

   x++;

 }while(x>12);

}

 

Ukiangalia hapo utaona ijapokuwa sharti halijafikiwa lakini code zetu zilianga ku run na kutuma matokeo 1*7= 7.

 

Mwisho:

Somo linalofuata tutakwenda kujifunza kuhusu break and continue kweny loop. Hivyo basi edelea kufanyia mazoezi kwa mifano zaidi.