Sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi.
1. Kwanza kabisa tunapaswa kufahamu kwamba mfuko wa kizazi yanani uterusi upasuka pale mama anapokuwa na uchungu, unaweza kupasuka mzima au akapasuka sehemu kidogo na mama akipata huduma ya haraka anaweza kutoa mtoto wake akiwa hai kabisa.
2. Sababu ya kwanza ni kuwepo kwa alama au kovu kwenye tumbo, kwa mfano labda mama kwenye mimba ya kwanza alifanyiwa upasuaji na akipatwa na uchungu akiwa mbali na hospitali na akakosa huduma ya haraka anaweza kupasuka mfuko wa kizazi.
3. Mtoto kushindwa kutoka kwenye via vya uzazi kwa kitaalamu huitwa obstructed labour kwa sababu pengine njia ni ndogo kwa hiyo mtoto ukaa humo na anajaribu kutoka lakini anashindwa na mda unaendeleaje bila msaada wowote hatimaye mfuko wa kizazi unapasuka.
4. Kusinyaa sana kwa mfuko wa kizazi.
Ili mama aweze kujifungua anapaswa kuwa na uchungu na uchungu huo utokea kwa sababu ya kusinyaa kwa mfuko wa uzazi, kuna kipindi uchungu inakosa na mama anapewa dawa aina ya oxytocin ambayo Usababisha kusinyaa kwa mfuko wa uzazi na ukisinyaa sana bila mpangilio usababisha kupasuka kwa mfuko wa uzazi.
,5. Kwa hiyo baada ya kuona sababu hizo tunapaswa kuzitambua na kuzielewa vizuri na kuokoa maisha ya Mama na mtoto ili kuweza kumfanya mama ajifungue kwa urahisi zaidi.