Jinsi ya Kutengeneza Folda, Faili, na Kuingiza Data kwa Python

Katika somo hili, utajifunza hatua kwa hatua jinsi ya kutengeneza folda (directory), faili, kuingiza data kwenye faili, na hata kufuta faili kwa kutumia Python.


1. Kutengeneza Folda

Katika Python, tunaweza kutumia moduli ya os kutengeneza folda. Ili kutengeneza directory, tunatumia method ya os.makedirs().

Mfano wa Kutengeneza Folda:

import os

# Kutengeneza folda mpya

os.makedirs('data', exist_ok=True)

print("Folda 'data' imetengenezwa.")

 

Ufafanuzi:


2. Kutengeneza Faili na Kuingiza Data

Baada ya kutengeneza folda, tunaweza kutengeneza faili na kuingiza data kwa kutumia mode ya write (w). Kwanza tutafunguwa hilo faili kwa kutumia open() baada ya kulifunguwa ndipo tutaandika data kwa kutumia write() 

Mfano:

# Kutengeneza faili na kuandika data

with open('data/tile.txt', 'w') as file:

    file.write("Karibu Bongoclass\n")

    file.write("Upate kujifunza mengi\n")

    file.write("Bila malipo\n")

 

print("Faili limeundwa na data zimeingizwa.")

 

 

Ufafanuzi:

 

Writing mode

Unaweza kujiuliza hiyo ( w) kwenye open() na write() ni nini hasa. Hapo imetumika kama writing mode, inaonyesha kwa namna gani hiyo function ifanye kazi. Kazi ya mode ya w ni kufunguwa faili a kuandika. Hata hivyo haipo peke yake zipo mode nyingine kama a, a+, b, w, w+, r, r+ angalia kazi za kila mode kwenye jedwali hapo chini

 


3. Kuingiza Data kutoka kwa Mtumiaji

Tunaweza kutumia input() kwa kuingiza data kutoka kwa mtumiaji na kuiandika kwenye faili.

Mfano:

# Kufungua faili kwa mode ya kuandika

with open('wanafunzi.csv', 'w') as file:

    file.write("Jina,Namba ya Simu\n")  # Kichwa cha faili (header)

 

    # Kuingiza majina ya wanafunzi watatu

    for i in range(3):

        jina = input(f"Andika jina la mwanafunzi wa {i + 1}: ")

        simu = input(f"Andika namba ya simu ya mwanafunzi wa {i + 1}: ")

        file.write(f"{jina},{simu}\n")

 

print("Faili la wanafunzi.csv limeundwa.")

 

Ufafanuzi:


4. Kufuta Faili

Ili kufuta faili, tunatumia method ya os.remove().

Mfano:

import os

# Futa faili

if os.path.exists('data/tile.txt'):

    os.remove('data/tile.txt')

    print("Faili 'tile.txt' limefutwa.")

else:

    print("Faili halipo.")

 

Ufafanuzi:


5. Kufuta Folda

Ili kufuta folda, tunatumia method ya os.rmdir(). Folda lazima iwe tupu kabla ya kuifuta.

Mfano:

import os

# Futa folda

if os.path.exists('data'):

    os.rmdir('data')

    print("Folda 'data' imefutwa.")

else:

    print("Folda haipo.")

 


Hitimisho

Hapo juu tumepitia hatua za:

  1. Kutengeneza folda.

  2. Kutengeneza faili na kuandika data.

  3. Kuingiza data kutoka kwa mtumiaji.

  4. Kufuta faili.

  5. Kufuta folda.

Python ni lugha yenye nguvu kwa usimamizi wa mafaili na folda, na moduli kama os na shutil hutoa zana rahisi za kutekeleza kazi hizi.

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata tutajifunza kusoma mafaili