Mambo muhimu anayofanyiwa Muislamu (mtu) anayekaribia kufa.
Mtu akikaribia kufa huwa hajiwezi kwa lolote lile pamoja na elimu, ujuzi alionao, hivyo huhitajia kufanyiwa mambo yafuatayo;
- Kuogeshwa, kugishwa mswaki na kumpaka mafuta au manukato kama kuna uwezekano.
- Kumlaza kwa ubavu wa kulia au chali na kumuelekeza Qibla iwapo kuna uwezekano.
- Kumpa maji ya kunywa.
- Kutamka (kumsomea) – Shahada “Laa ilaha illallaah”
Abu Said na Abu Hurarirah wamesimulia kuwa, Mtume wa Allah amesema: “Wasomeeni watu wenu wanaokaribia kufa; ‘Laailahaillallaah”
Pia Mu’az bin Jabal amesema kuwa Mtume (s.a.w) amesema: “Yule ambaye maneno yake ya mwisho yatakuwa; “Laailahaillallaah” ataingia peponi.
(Abu Daud)
- Si lazima anayekufa aitamke kwa sauti, inaweza ikawa kimoyo moyo