Swali: Nini maana ya Elimu na ni nani aliye elimika?
Jibu:
- Katika Uislamu Elimu maana yake ni:
- Ujuzi unaoambatana na utendaji au
- Mabadiliko ya tabia yanayoambatana (yanayotokana) na ujuzi au
- Ujuzi unaomuwezesha mtu kufanya (kutenda) jambo kwa ufanisi au inavyotakikana.
- Nani aliyeelimika? (Sifa za mtu aliyeelimika).
- Aliyeelimika ni yule mwenye ujuzi unaomuwezesha kutenda (kufanya) jambo kwa ufanisi na inavyotakikana.
- Mjuzi wa Qur’an na Sunnah ni yule anayeendesha kila kipengele cha maisha yake ya binafsi na kijamii kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah.
- Watakapo fanana kimwenendo na kitabia wale wenye elimu na wasiokuwa na elimu, basi wenye elimu watakuwa hawajaelimika ila wamesoma tu.
“……………Sema, Je! Wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua? Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu………”(39:9).