Mafunzo yatokanayo na Mikataba ya ‘Aqabah katika kuandaa ummah.
- Waislamu hawana budi kupanga mikakati na mambo yao kwa siri ili kutojulikana na maadui wa Uislamu na waislamu.
- Waislamu hawanabudi kutotangaza mikakati yao kwa maadui kabla ya kuitekeleza ili kuepukana na njama ya kukwamishwa.
- Waislamu hawanabudi kuwa na mipango na mikakati (long and short term strategies) ya muda mrefu na mfupi katika kuandaa Ummah.
- Uongozi bora na makini ni jambo la msingi sana la mwanzo katika kuusimamisha na kuuendeleza Uislamu katika jamii.
- Waislamu wanaharakati wanapoazimia jambo lolote katika kuusimamisha na kuuendeleza Uislamu, hawana budi kujifunga nalo na kupeana kiapo cha utekelezaji.
- Waislamu hawana budi kutumia kila aina ya fursa itakayojitokeza katika kuusimamisha na kuuendeleza Uislamu katika jamii.