Assignment operator:

Hizi ni zile operator ambazo hutumika ku assign thamani kwenye variable, yaani kuipa variable thamani. Kama unaposema x = 2 hapo assignment operator (=) imetumika kuipa x thamani yake. 

Mifano ya assignment operator:-

  1. Alama ya (=) mfano a = 3
  2. Alama ya (+=) mfano a += 3 hii ni sawa na kuandika a = a+3
  3. Alama ya (-=) mfano a -=3 hii ni sawa na kuandika a = a-3
  4. Alama ya (*=) mfano a *=3 hii ni sawa na kundika a = a *3
  5. Alama ya (/=) mfano a /=3 hii ni sawa na kuandika a = a/3
  6. Alama ya (%=) mfano a %3 hii ni sawa na kuandika a = a %3


 

Logical operator:

Hizi hutumika kuweka logical kwenye variable ama thamani

  1. && huitwa logical and alama hii kwenye programming inamaanisha and yaani “na” . yenyewe italeta jbu true kama statement itakuwa kweli na kinyume chake. Mfano 2 ni kubwa kuliko 1 na 3 kubwa kuliko 2. Sasa haya melezo yote ni sawa hivyo jibu ni true. Maelezo haya unaweza kuyaandika hivi:  2 > 1 && 3>2

 

  1. || huitwa logical or alama hii ina aana or  yaan “au” hii itatoa jibu true kama moja ya statement ni kweli mfano 2 ni kubwa kuliko 5 au 6 ni kubwa kuliko 5. Hapa statement ya kwanza sio kweli, lakini ya mbili ni kweli, hivyo kwa ujumla tutapata jibu true kwa kuwa moja ya statement ni true. Maelezo haya tunaweza kuyaandika hivi 2 > 5 || 6>5

 

  1. ! huitwa logical not kazi yakeni kukataa statement, kama ni ya ukwei inakuwa ni uongo. Mfano tunajuwa kuwa 5 ni sawa na 5 hivyoukiandika hivi 5 ==5 hi ni true. Lakini kama nitaweka logical not itamaanisha 5 sio sawa na 5 yaani 5 !=5 hapa jibu litakuwa ni false kwa kuwa sio kweli.

 

print(5!=5)

 

 

Identity operator:

Operator hizi zina kazi ya kuangalia ama kulinganisha kama value mbili zote zinaelekea kwenye object moja. Mfano wa operator hizi ni is na is not.

Mafno:

a = 3

y = a

print(a is y)

 

Hii itakupa jibu la true  kwa kuwa weote x ya y wanawakilisha object moja a,bayo ni namba 3.

 

Na kama nitageuza kutumia is not  nitapata jibu false 

a = 3

y = a

print(a is not y)

 

 

Membership operator

Hii kazi yake ni kuangalia je mtiririko wa string (sequence of string) unapatikana kwenye hiyo objects.operator hizi ni in na not in. Zenyewe zitatoa jibu true  kama hizo string zipo na false kama hazipo. 

 

Mfano ninastring hii “haloo karbu bongoclass ujifunze python bure” sasa katika strng hii nataka kuangalia kama neno python  lipo ama halipo.

text = "haloo karbu bongoclass ujifunze python bure"

print("python" in text)

 

Hapo tutapata jibu true kumaanisha kuwa neno python  lipo. Na kama unataka kuangalia kama halipo utatumia not in. Sasa in not uaangalia je hilo neno halipo kweli, kama halipo utapata jibu true. Kwa mfano wetu hapo juu tutapata jibu false kwa sababu neno lipo

text = "haloo karbu bongoclass ujifunze python bure"

print("python" not in text)


 

Mwisho:

Katika somo linalofuata utakwenda kujifunza kuhusu String kwa undani zaidi.