SWALI

Habari ndugu mi nipo na swali nahitaji msaada je, unaweza kupata ujauzito bila kupata hedhi miezi 9 baada ya kujifungua mtoto? 

 

Jibu :

Swali la muulizaji jibu lake linatosha kuwa ndio.  Ni kweli kabisa unaweza pata ujauzito bila ya kuona hedhi baada ya kujifunguwa. 

 

Baada ya kujifungua kwa baadhi ya wanawake hukaa wiki 6 ndipo wapate hedhi,  wengine huchukua miezi 6 hadi kupata hedhi. 

 

Wakati wa kunyonyesha mwili huzuia homoni zinazokomaza mayai zisizalishwe.  Hii husaidia kutopata mimba. Kipindi hiki huathiriwa pia na aina ya unyonyeshaji. 

 

Sasa kuna baadhi ya wanawake hao huanza kukomaa kisha hedhi Inafuatia na wengine itaanza hedhi kisha yai litafuatia katika mzunguko ujao. 

 

Hivyo basi kama mwanamke yupo kwenyebkundibhili la ambao yai linatangulia kisha hedhi anaweza apate ujauzito na asijuwe na hedhi asipate,  kwa sababubakishapata mimba hatoweza tena kupata hedhi.