JAVASCRIPT FUNCTIONS:
Function ni kundi la code ambalo unaweza kulitumia zaidi na zaidi. Na hata hivyo function haiwezi kufanyakazi hata mpaka iwe imeitwa (invoked/called).
Function zipo katika namna mbili ambazo ni built in functions na user defined functions. Hizi built in function ni zile ambazo zimetengenezwa moja kwa moja na walioivumbuwa hii language. Na Usher defined function ni zile ambazo mtumiaji anazitengeneza yeye mwenyewe.
Jinsi ya kutengeneza function:
Iili kuweza kuandika function javascript hutumia keyword function kisha hufuatiwa na jina la function kisha hufuatiwa na mabano () ambayo ndani yake kunakaa parameta. Endapo zitakuwepo parameta zaidi ya moja utazitenganisha na alama ya kima, baada ya kuweka hayo mabano yenye parameta utaweka mabano mengine hay {} ambayo ndani yake ndio hukaa hizo cede za function yako.
Wacha tuone mifano ya functiona hapo chini: -
Mfano 1:
<!DOCTYPE html>
<html>
<head>
<title> Mfano wa 1 </title>
</head>
<body>
<script>
/* Mwanzo wa function */
function karibu(str) {
/* Code za function hukaa hapa */
document.write("Karibu Bongoclass");
}
/* Hapa ndipo utaiita function */
karibu();
</script>
</body>
</html>
Mfano 2:
Katika function pia tunaweza kutumia return keyword. Hii hutumika pale unapotaka kupata thamani ya fulani kutoka kwenye function yako.
Kwa mfano unafanya usajili wa watoto, hivyo unataka kuandika jina la mtoto, la bana ama ukoo pamoja na kabila lake. Unaweza kutumia return keyword ili kupata taarifa za mtoto huyu.
Keyword hii hasa hutumika kustop code zisiendelee ku run kisha huleta matokeo ya code hizo popote pale zilipoitwa.
<!DOCTYPE html>
<html>
<head>
<title>Mfano 2</title>
</head>
<body>
<script>
function usajili(jina, ukoo, kabila) {
return jina + " " + ukoo + " " + kabila;
}
var jina = usajili("Sayona", "Danis", "mzaramo");
document.write(jina);
</script>
</body>
</html>
Mfano 3:
Unaweza pia kutumia function kwa ajili ya kufanya mahesabu.
<!DOCTYPE html>
<html>
<head>
<title> Mfano 3</title>
</head>
<body>
<script>
function jumlisha(num1, num2) {
var jumla = num1 + num2;
return jumla;
}
/* function insitea hapa */
document.write(jumlisha(700, 300));
</script>
</body>
</html>
Kama ilivyo kwenye programming language zingine kuwa function zipo katika namna kuu 2 ambazo ni built -in- function na user defined function. Hapo juu nimeeleza jinsi ya kutengeneza function yako mwenyewe. Sasa mfano wa hapo chini nakuletea mfano wa built in function yaani function ambazo zimewekwa tayari na walioitengeneza javascript.
Mfano 4:
<!DOCTYPE html>
<html>
<head>
<title> Mfano 4</title>
</head>
<body>
<script>
document.write(eval(2+4));
</script>
</body>
</html>
Mwisho:
Somo linalofuata tutakuja kusoma kuhusu javascript object na jinsi ya kuzitengeneza hizo object. Kabla ya kusoma somo hili hakikisha umefahamu somo la 8 kipengele cha object.