Somo hili linaumuhimusana kwani wakati mwingineunapewa code za app ambazo zipo tayari. So itakubidi ujuwe jinsi ya kubadilisha jina, package name na baadhi ya config nyingine ili uweze kutengeneza app yako mwenyewe.
Jinsi ya kubadilisha jina:
Kwa app za android:
Nenda kwenye folder la Android -> app -> src -> main
-
Nenda kwenye faili linaloitwa AndroidManifest.xml
-
Funguwa hilo faili kisha tafuta palipo andikwa android:label
-
Mbele ya hayo maneno utaona jina la app limezungukwa na alama za funga semi yaani “” kwa mfano kwa mimi hapa ipo hivi android:label="mafunzo" sasa ondosha hilo jina uliolikuta kisha weka unalolitaka. Kwa mfano mimi ninaweza Bongoclass kwa hivo itaonekana hivi android:label="Bongoclass"
-
Mpaka kufikia hapo umeshabadili jina la app kwnee android.
Kwa app za ios:
-
Nedna wenye folder la ios-> Runner
-
Bofya fal lnalotwa info.plist
-
Funguwa faili hilo kisha tafuta palipoandikwa <key>CFBundleDisplayName</key> na <key>CFBundleName</key> chini ya mistari hiyo utakuta kuna jina la App. hapo utabadili kulingana na jina unalotaka. Kwa mfano imi nataka kuweka jina Bongoclass hivyo itakuwa hivi
<key>CFBundleDisplayName</key>
<string>Bongoclass</string>
<key>CFBundleName</key>
<string>Bongoclass</string>
Baada ya hapo run app yako kuona kama jina limeshabadilika.
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwennda kujifunza jinsi ya kubadilisha package name (app id) kwenye app ya flutter.