Kuna aina mbili za kuweka picha kwenye App ya flutter. Kwanza ni picha ya offline, picha hii unaiweka kwenye app yako kama mafaili mengineyo. Njia ya pili ni kuweka picha ambayo ipo online hivyo tunatumia link ya picha hiyo kwenye App yetu.

 

Property za Image:

1. image: (property hii ni lazima kuwepo) Inabainisha picha itakayotolewa. Unaweza kutumia aina ya ImageProvider kama vile AssetImage, NetworkImage, au FileImage kama chanzo cha picha.

 

2.width: Inabainisha upana wa picha. Unaweza kutoa thamani ya double kuweka upana wa picha kwa pikseli za mantiki.

 

3.height: Inabainisha urefu wa picha. Unaweza kutoa thamani ya double kuweka urefu wa picha kwa pikseli za mantiki.

 

4.fit: Inadhibiti jinsi picha itakavyoingizwa ndani ya nafasi yake. Thamani zinazowezekana ni:

 

5.BoxFit.contain: Inapanua picha ili kuingiliana na chombo huku ikidumisha uwiano wake wa asili.

BoxFit.cover: Inapanua picha ili kufunika kontena lote, ikikata ikiwa ni lazima.

BoxFit.fill: Inayeyusha picha ili kujaza kontena lote, ikivuruga uwiano wake wa asili.

BoxFit.fitWidth: Inapanua picha ili ifanane na upana wa kontena huku ikidumisha uwiano wake wa asili.

BoxFit.fitHeight: Inapanua picha ili ifanane na urefu wa kontena huku ikidumisha uwiano wake wa asili.

BoxFit.none: Haina mabadiliko yoyote kwenye ukubwa wa picha.

 

6.alignment: Inabainisha usawazishaji wa picha ndani ya nafasi yake. Thamani inapaswa kuwa ya aina ya Alignment na inaweka picha ndani ya chombo.

 

7.color: Inatumia kichujio cha rangi kwa picha.

 

8.colorBlendMode:  Inabainisha jinsi rangi iliyowekwa na property ya color itakavyochanganywa na picha.

 

9.repeat:  Inabainisha jinsi picha itakavyorudi ikiwa haijaijaza nafasi yake kikamilifu.

 

Jinsi ya kuweka Picha:

Sasa ili tuweke picha tutatumia ImageProvider ambazo nimezitaja kwenye property ya image. Ambazo ni asset na network

 

  1. Kwa kutumia AssetImage

Kwa kutumia jia hii utaweza kutumia faili ambalo utaliweka kwenye app yako. Hivyo kwanza utafuata njia hizi:-

  1. Kwanza ingia kwenye folder la project yako. Folda lenyewe ambalo kuna mafaili mengine kama pubspec.yaml
  2. Utatengeneza folda hapo lipe jina la assets. Unaweza kuweka jina lolote unalotaka. Ndani ya foler hili tengeneza folda linguine liite images pia unawez akuweka jina unalolitaka wewe. Sasa ndani ya folda la images hapo weka picha zako unazotaka zionekane.
  3. Hatuwa inayofuata nenda kwenye faili linaloitwa pubspec.yaml  kisha tafuta mstari ulioandikwa flutter: na hakuna mwingine wenye jina hilo kuelekea chini. Maana mistari yenye flutter ipo mingi ila tafuta ambazo ni wa mwisho. Kisha weka code hizi

assets:

 - assets/images/

Weka kama unavyoziona hapo kwa mtiririko huohuo. Code hizi zinasajili folda letu la assets ambalo lina folda la picha. Baada ya hapo sasa tutakuwa tayari kuweza kutumia picha yetu kwenye App.kuna  worning unaweza kuziona kwenye faili la main.dart. Bofya hizo warning kupata maelekezo zaidi.

 

Sasa ili tuweze kutumia picha tutatumia widget ya picha ikifuatiwa na image provider. Mfano

Image.asset("images/bongo.png")

 

Code nzima hizi hapa

import 'package:flutter/material.dart';

 

void main() => runApp(MyApp());

 

class MyApp extends StatelessWidget {

 @override

 Widget build(BuildContext context) {

   return MaterialApp(

     home: Scaffold(

       appBar: AppBar(

         title: Text("image assets"),

       ),

       body: Center(  // Center the image on the screen

         child: Image.asset("images/bongo.png"),

       ),

     ),

   );

 }

}

 

Sasa hapo unaweza kutumia property tulizozitaja hapo juu kuweza kuboresha muonekano wa picha yako. Wacha tuone mfano.

 

Kuweka height na width yaani upana na urefu

 

import 'package:flutter/material.dart';

void main() => runApp(MyApp());

class MyApp extends StatelessWidget {

 @override

 Widget build(BuildContext context) {

   return MaterialApp(

     home: Scaffold(

       appBar: AppBar(

         title: Text("image assets"),

       ),

       body: Center(  // Center the image on the screen

         child: Image.asset(

           "images/bongo.png",

           width: 20, // Set the width to 200 logical pixels

           height: 200, // Set the height to 200 logical pixels

         ),

       ),

     ),

   );

 }

}

 

 

 

Kwa ktumia network image

Sasa ttakwenda kuweka picha ambayo ipo kwenye website fulani kwenye App yetu. Mfano kuna link hapa https://picsum.photos/250?image=9

Hii itatupa picha hii

 

Sasa tunataka picha hii kuieweka kwenye app yetu. Sasa hatuna tena haja ya kufanya setting kwenye faili lolote lile. Tutakachofanya ni hiki Image.network("https://picsum.photos/250?image=9")

 

Hapo moja kwa moja picha yetu itasoma kwenye App yetu. Zingatia kuwa picha inatakiw aiwe inapatikana kwenye internet.

import 'package:flutter/material.dart';

 

void main() => runApp(MyApp());

 

class MyApp extends StatelessWidget {

 @override

 Widget build(BuildContext context) {

   return MaterialApp(

     home: Scaffold(

       appBar: AppBar(

         title: Text("Image from URL"),

       ),

       body: Center(  // Center the image on the screen

         child: Image.network("https://picsum.photos/250?image=9"),

       ),

     ),

   );

 }

}

 

 

 

 

Mwisho:

Katika somolinalofuata tutakwenda kujifunz ajisni ya kutumia icon, kwenye App yako. Ijaokuwa tumeshatumia icon, mfano katika somo la batani kuna icon tuliweza kuzitumia.hivyo somo linalofuata utakwenda kujifuza uwekaji wa icon.