UTANGULZI:
Flutter ni mfumo wa maendeleo wa programu iliyotengenezwa na Google kwa ajili ya kuunda programu za rununu, wavuti, na desktop kwa kutumia lugha ya Dart. Ni mfumo wa "cross-platform" ambao inaruhusu waundaji wa programu kujenga programu moja na kupeleka kwa vifaa mbalimbali kama vile simu za mkononi zinazotumia mfumo wa Android na iOS, kompyuta za mezani, na hata wavuti za kawaida.
Kwa kutumia Flutter, waundaji wa programu wanaweza kuunda programu zenye muonekano mzuri na wa kuvutia kwa kutumia seti ya vifaa vya kutengeneza (widgets) ambavyo vinaweza kubadilishwa kwa urahisi na kuunganishwa pamoja kwa njia ya kujengwa kwa kasi na yenye ufanisi. Flutter pia hutoa uwezo wa kasi ya utendaji na utangamano wa hali ya juu kwa kusudi la kuwa na programu zenye utendaji mzuri sana.
Kwa kifupi, Flutter ni chombo bora kwa waundaji wa programu ambao wanataka kuunda programu zenye muonekano mzuri, kazi bora, na utendaji wa hali ya juu kwa vifaa mbalimbali.
Flutter ilianzishwa na Google. Ilitangazwa kwa mara ya kwanza na Google mnamo Mei 2017 katika hafla ya Google I/O. Baadaye, ilifanywa kuwa chanzo wazi mnamo Desemba 2018. Hii iliruhusu jamii ya maendeleo kushiriki katika maendeleo ya Flutter na kuchangia kwenye mradi. Tangu wakati huo, Flutter imekuwa maarufu sana na imekuwa chaguo kuu kwa waundaji wa programu wanaotaka kujenga programu za rununu, wavuti, na desktop kwa kutumia lugha ya Dart.
Jinsi ya kuandaa kifaa chako:
Hapa nitakufunza jinsi ya kuandaa kifaa chako kwa ajili ya somo hili.
- Kwanza utahitajika ku download flutter SDK:
Ili uweze ku download flutter SDK ingia kwenye website ya flutter flutter.dev
- Kisha utachaguwa platform unayotumia. Kama unaumia window bofa kweye window, ama vinginevyo.
- Baada ya hapo utacaguwa tena aina ya app unayotaka kutengeneza. Chaguwa mobile kama lengo lako ni kutengeneza app za simu
- Kisha utaletewa tena ukurasa shuka mpaka palipoandikwa install the flutter SDK hapo bofya palipoandika Download then install hapo uta dowmload faili lililopo katika mfumo wa zip. Utakachofaya ni ku unzip na kuliweka folder sehemu rahisi kufikika. Kwa mfano mimi nimeweka kwenye disk C kwenye user. Na nimelita flutter.
Hatuwa inayofuata ni ku add environment variable:
Nenda kwenye folda la flutter kisha nenda kwenye folder la bin. Kisha copy link ya hiyo location. Angalia kwenye channel yetu ya youtube jinsi ya kupata folder location.
Kisha ndenda kwenye setting tafuta envronment variable, kisha bofya edit environment variable kisha bofya palipoandikwa path. Kisha bofya new, hapo pest link ulioikopi kwenye hatuwa ya hapo juu. Baada ya apo apply na save.
Hatuwa inayofuata ni ku install android studio na kuweka flutter plugin
Ingia kwenye website ya android hapa kisha download toleo jipya la android studo. Kisha install. Hakikisha una bando kama GB mbili kama ndio kwanza una install android studio. Baada ya kumaliza ku install ifunguwe kisha itakapo funguka bofya palipoandika plugin. Tafuta flutter kisha bofya install. Kisha tafuta dart kisha bofya install. Baada ya hapo restart hiyo android studio yako. Itakapofunguka utaona sasa kuna menu inayosema New flutter project.
Mwisho:
Somo linalofuata tutajifunza jisni ya kutenegeneza App yetu ya kwanza. Tafadhali angalia video yetu upate kuona kwa vitendo.