Utangulizi
Hawariyuna walikuwa wafuasi wa karibu wa Nabii Isa (a.s.) waliomsadia kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu. Walijulikana kwa kusalimisha nafsi zao kwa Allah na kwa kumtii Mtume wake. Katika Qur’an, dua zao zimetajwa ili kutufundisha mafunzo ya subira, imani ya dhati na kujisalimisha kwa Allah.
maudhui
-
dua ya kuomba kujumuishwa na mashahidi
رَبَّنَا آمَنَّا بِمَا أَنْزَلْتَ وَاتَّبَعْنَا الرَّسُولَ فَاكْتُبْنَا مَعَ الشَّاهِدِينَ
(Āl-ʿImrān 3:53)Tafsiri ya Kiswahili:
“Mola wetu Mlezi! Tumeyaamini uliyo yateremsha, na tumemfuata huyu Mtume, basi tuandike pamoja na wanao shuhudia”Hii inaonyesha imani ya Hawariyuna kwa wahyi wa Allah na ufuasi wao wa dhati kwa Nabii Isa (a.s.). Waliomba wasiwe tu waumini wa kawaida, bali waandikwe miongoni mwa mashahidi wa ukweli wa dini.
-
dua ya kuomba meza kutoka mbinguni (Dua hii aliomba Nabii Isa pindi wanafunzi wake walipohitaji miuziza)
اللَّهُمَّ رَبَّنَا أَنزِلْ عَلَيْنَا مَائِدَةً مِّنَ السَّمَاءِ تَكُونُ لَنَا عِيدًا لِّأَوَّلِنَا وَآخِرِنَا وَآيَةً مِّنكَ ۖ وَارْزُقْنَا وَأَنتَ خَيْرُ الرَّازِقِينَ
(Al-Mā’idah 5:114)Tafsiri ya Kiswahili:
“...Ewe Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wetu! Tuteremshia chakula kutoka mbinguni ili kiwe Sikukuu kwa ajili ya wa mwanzo wetu na wa mwisho wetu, na kiwe ni Ishara itokayo kwako. Basi turuzuku, kwani Wewe ndiye mbora wa wanao ruzuku..”Dua hii inaonyesha uhitaji wa Hawariyuna wa dalili ya dhahiri kutoka kwa Allah, na pia shukrani yao kwa neema ya chakula na riziki.
matumizi ya dua hizi katika maisha ya kila siku
-
Imani thabiti: Dua ya kwanza inatufundisha kuomba uthabiti katika imani na kuhesabiwa miongoni mwa mashahidi wa haki. Katika maisha yetu ya kila siku, tunaweza kuiomba Allah atufanye mashahidi wa haki kazini, majumbani na katika jamii.
-
Shukrani na riziki: Dua ya pili inatufundisha kumshukuru Allah kwa riziki na kuomba kila tunachopata kiwe ni baraka. Katika maisha ya kila siku, tunaweza kuitumia tunapopokea neema, au tunapotaka riziki yenye baraka.
hitimisho
Dua za Hawariyuna zinatufundisha misingi miwili mikuu: kuamini kwa dhati na kushukuru neema za Allah. Waliomba kwa unyenyekevu, wakitambua udhaifu wao na kuonyesha utiifu wao kwa Nabii Isa (a.s.). Hii ni funzo kwetu kwamba dua ni chombo cha kuimarisha uhusiano wetu na Allah katika kila hali.