Kutengeneza folder:

Katika programming folda linaitwa directory. Hivyo ili tuweze kutengeneza directory tutatumia function ya Directort() function hii tutaweka jina la directory kama argument yake. Kisha tutatumia method ya crete(). Mfano tunakwenda kutengeneza folda tunatakaloliita data.

import 'dart:io';

void main(){

 Directory('data').create();

}

 

Kutengeneza faili na kuweka data

Hapa tutatengeneza faili kwenye folda letu tuliotengeneza hapo juu. Ili kutengeneza faili tutatumia function ya File() ambapo jina la faili na jina la folda utaweka ndani kama argument.

 

Kwanza tutatengeneza variable yetu. Kenyr data type yake weka File

Mfano variable nitaiita faili_letu

File file_letu = File('data/tile.txt');

 

Kisha tutatumia function ya  writeAsStringSync()      kuungiza data kwenye faili letu. Ndani ya function hiyo ndipo utaweka data kama argument. Mfano faili letu litakuwa na data hizi

Karibu Bongoclass

Upate kujifunza mengi

Bila malipo

 

import 'dart:io';

void main(){

 File file_letu = File('data/tile.txt');

 file_letu.writeAsStringSync('Karibu Bongoclass Upate kujifunza mengi Bila malipo');

print('faili limetengenezwa');

}

 

Sio lazima kuweka folda hapo, unaweza kutengeneza faili popote pale. Mfano faili letu tunakwenda kuliweka pamoja na orodha nyingine za mafaili kwenye root folder

import 'dart:io';

void main(){

 File file_letu = File('tile.txt');

 file_letu.writeAsStringSync('Karibu Bongoclass Upate kujifunza mengi Bila malipo');

print('faili limetengenezwa');

}


 

Pia tunaweza kutumia input data. Sasa hapa tutakwend akutumia mode: FileMode.append

Kwa ajili ya kusubiria loop. Tunakwenda kutumia loop kwa ajili ya kuingiza majina ya wanafunzi watatu. Watakapotimia watatu ukibofya enter ndipo faili litatengenezwa. Kufanya hivi ndipo tutatumia append  mode

// dart program to write to csv file

import 'dart:io';

 

void main() {

 // funguwa au tengeneza faili file

 File file = File("wanafunzi.csv");

 // andika data

 file.writeAsStringSync('Jina,Simu ');

 for (int i = 0; i < 3; i++) {

   // ingiza jina

   stdout.write("Andika jina la mwanafunzi wa ${i + 1}: ");

   String? jina = stdin.readLineSync();

   stdout.write("Andika namba ya mwamnafunzi wa  ${i + 1}: ");

   // andika namba ya simu

   String? simu = stdin.readLineSync();

   file.writeAsStringSync('$jina,$simu ', mode: FileMode.append);

 }

 print("gaili la csv limetengenezwa");

}

 

Kama utalifunguwa hilo faili kwa kutumia microsoft office excel itakuletea data kama hivi

Kufuta faili

Sasa ngoja tujifunze kututa faili. Kufanya hivyo utatumia function ya deleteSync().

import 'dart:io';

 

void main() {

 // Fungua faili

 File file = File('tile.txt');

 // Futa data

 file.deleteSync();

 print('Faili limefutwa');

}

 

Utaona hapo faili la tile.txt halipo tena.

Pia unaweza kuangalia kama faili lipo ama halipo kabla hujajaibu kulifuta. Kufanya hivi tutatumia function ya deleteSync()

import 'dart:io';

 

void main() {

 File file = File('tile.txt');

 if (file.existsSync()) {

   file.deleteSync();

   print('Faili limefutwa.');

 } else {

   print('faili halipo.');

 }

}

 

Hapo kama utatumia tile.txt utaona utaambiwa kuwa faili halipo.

 

Mwisho:

Huu ndio mwisho wa course ya DART level 1, sasa somo linlofuata tutakwenda kuanza OOP yaani Object Oriented Programming kwenye Dart.