Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu class kwenye Dart OOP. utajifunza sintaksia zake na jinsi ya kuweza kuitumia.

 

Nini maana ya class 

Kwenye OOP class ni blueprint kwa ajili ya kutengeneza object. Lamda nitoe mfano upate kuelewa. Kwa mfano tunakuwa na class yetu inatwa gari kisha gari linakuwa na sifa zake na tabia zake. Kwa mfano gari lina rangi, milango na matairi hizi ji attribute za class yetu inayoitwa gari. HAlafu class yetu gari ikawa na tabia kama inatembea kwa haraka, ni ndogo, na ni nyepesi hizi ni behaviour yaani tabia. Katika course hii tutakwenda kutumia mfano wa gari.

 

Sasa kwa kuwa class yetu gari tumesha itengenezea tabia na sifa zake. Sasa tunapotaka kutengeneza object yeyote inayohus gari inakuwa na sifa hizo. Mfano object toyota katika sifa iiatkuwa na rangi nyeusi, milango miwili, na matairi 4, na katika tabia itakuwa ni ndogo, na ni nyepesi. 

 

Sasa kila unapotengeneza object lazima ufuate sifa hizo. Iwe ni toyota, BMW, bugati ama object yeyote ambayo ni gari. Ndio maana tunasema class ni blueprint kwa maana object zote zitafuata mpangilio uleule wa class husika. Ni sawa na kufananisha class na ramani ya nyumba. Kwa maana nyumba itafuaa kama ramani inavyotaka.


 

Jinsi ya kuandika class.

Ili uweze kutengeneza Class tutatumia keyword class ikifuatiwa na jina la hiyo class mfano gari kisha itafuatiwa na mabano {} ambapo ndani yake kutakaa code za hiyo class.

Mfano:

class gari{

 

}


 

Sehemu iliyo ndani ya mabano {} ndio huitwa  body of the class hapa ndipo ambapo utaweka hizo code za class. Miongoni vya vitu muhimu vitakaa hapo ni properties na function.

 

Properties hizi ni kama variable hutumika kuhifadhi data, pia hutambulika kama fields au attributes. Na function hutumika kufanya matendo mbalimbali. Pia functions hutambulika kama methods.

 

Wacha tuone jinsi ya kuandika class yenye method na properties

class gari{

//properties

String? jina;

String? rangi;

int? matairi;

 

//method

void tangazo(){

 print("tunauza gari aina ya ${jina}, ina rangi ${rangi}, na matairi ${matairi}");

}

}


 

Mpaka kufikia hapo tumeweza kutengeneza class yetu pamoja na kuweka method ambayo tutaitumia ili kuweza ku print tangazo letu la kuuza gari. Sasa code hizo haziwezi kurint kitu chochote kwa sababu hatujatengeneza object.Pia tutatakiwa kutengeneza properties za object. 

 

Wacha tuone mfano mwingine wa class inayoitwa website yenye properties kama jina, category, status na mwaka ilipo anzishwa.

class website{

 var jina;

 String? status;

 String? category;

 int? creted;

 

 taarifa(){

   return "Jina la website yetu ni ${jina}, imeanzishwa mwaka ${creted}, hali yake kwa sasa ni ${status}, website yetu inahus ${category}";

 }


 

Nakwenda kuandika class nyingine ambayo itakwenda kuwa na function inayokubali parameter mbili.

class math{

 int? x;

 int? y;

 

 jumlaisha(x, y){

   return x+y;

 }

 

Mwisho:

Katika somo linalofuata tutakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza object pamoja na kuweka properties kwenye hiyo object, kisha tutaprint matokeo ya code zetu.