Library ni nini?
Library ni mkusanyiko wa programming instruction yaani ni yale maelekezo ambayo huamrishwa kompyuta kuyafuata. Dart yenyewe ina library zake. Kwa mfano wakati tunajifunz akuhusu mahesabu tulitumia library ya math ambapo tuli import kwa kutumia import 'dart:math';Pia wakati tunataka kupata user input tulitumia library ya io ambayo tuli import kwa kutumia import 'dart:io';Pia huko mbele tutakwenda kutumia html kwenye dart tutatulia library ya html kw akutumia import 'dart:html';
Hizi library zipo tu nyingi na kila moja ina matumizi yake mengi tu. Kwa muda wako unawez akuzifuatilia dart library kwenye website yao ya Dart, link nimetoa kwenye somo la kwanza.
Jinsi ya kutengeneza library yako mwenyewe.
Ili uweze kuetengeneza library kwanza utatengeneza faili lingine kisha utaliba jina unalolotaka kwa mfano tutatengeneza faili tutaliita hesabu.dart
Ndani ya hilo faili mstari wa kwanza anza na kuandika keyword library ikifuatiwa na jina la hiyo library. Mfano hesabu
library hesabu;
Sasa chukulia tunataka library yetu ya hesabu iweze ktafuta eneo la pembe tatu, eneo la mraba na eneo la trapeza. Tutatumia kanuni zile zile za darasa la 5 shule ya msingi. Eneo la pembetatu ni (kimo * kitako) ½ eneo la mraba ni (urefu * upana) na eneo la trapeza ni ((a +b) *h / 2)
Sasa kanuni hizi kila moja wapo hapo tanakwenda kuitengenezea function yake ili kuweza kufanya kazi husika.
library kanuni;
pembe_tatu(int h, int b) {
return (h * b )* 1 / 2;
}
mraba(int w, int h){
return w *h;
}
trapeza(int a, int b, int h){
return ((a +b)*h)/2;
}
Sasa ili tuweze kuitumia library tetu tutakwend aku import kwenye failia mbalo tunataka kuitumia. Katika ku import tutafanya kama tulivyofanya kwenye library nyingine. Kikubwa zingatia jina la faili.
import 'hesabu.dart';
void main(){
var eneo_la_pembetatu = pembe_tatu(20, 4);
var eneo_la_mraba = mraba(7, 7);
var eneo_la_trapeza = trapeza(10, 7, 5);
print('eneo la pembe tatu ni ${eneo_la_pembetatu}');
print('eneo la pembe mraba ni ${eneo_la_mraba}');
print('eneo la pembe trapeza ni ${eneo_la_trapeza}');
}
Kwa namna kama hiyo unawez akutengeneza library yako ili kufanikisha utendaji kazi wa project yako.
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwend akujifunza jinsi ya kutumia html kwenye Dart.