- Kukadiria namba
Chukulia mfano 10/3 = 2.5. Sasa tukiikadiria hapa tutapata 3
void main(){
double jibu = 10/4;
print(jibu);
print(jibu.round());
}
- Kuangalia sifa za namba
- Namba shufwa (isEven)
Hii itatoa jibu true ikiwa kweli na false ikiwa si kweli. Washa tutest kama 4 ni shufwa
void main(){
print(4.isEven);
}
True
- Kutengeneza hashcode ya namba (hashCode)
Hii itakuletea hashcode ya namba husika. Kwa mfano namba 5 tunakwenda kuitengenezea hashcode haye
void main(){
print(5.hashCode);
}
58005
- Kunagalia kama namba ni hasi tutatumia isNegative
- Kuangalia kama namba ni infinit - haina mwisho tutatumia isInfinit
- Kuangalia kama namba ni finit - ina mwisho tutatumia isFinit
- Kuangalia kama namba sio negative - hasi tutatumia isNan
- Kuangalia kama namba ni witiri yaani odd tutatumia isOdd
3. Kubadili namba kuwa string toString
void main(){
print(4.toString());
}
4
Zipo method nyingine za namba. Sasa nataka tuhame tuingie kwenye library ya math yaani math library.
Math library
Ni mkusanyiko wa tools za kufanyia mahesabu. Tutakwedna kujifunza vyema katika somo la library. Hapa ninachotaka ni uweze kujifunza kuitumia library ya mahesabu.
Kwanza tutatakiwa ku import hii library kama tulivyofanya kwenye dart:io. Ku import math library tutatumia import 'dart:math';Kisha library itakuwa tayari kuweza kutumiwa.
Mfano:
Tunataka kutafuta 2 kipeuo cha tatu yaani 2 power 3 (23 ) kufanya hivi tutatumia pow()
import 'dart:math';
void main()
{
print(pow(2, 3));
}
8
Mfano
Tuna namba mbili 2 na 3 sasa tunataka kutafuta namba kubwa ni ipi na ndogo ni ipi. Hapa tutatumia min() na max()
import 'dart:math';
void main()
{
print(max(2, 3));
print(min(2, 3));
}
3
2
Mfano
Tunataka kutafura square root ya namba kwa mfano 49 ambapo nisawa na kusema 7 *7 = 49
import 'dart:math';
void main()
{
print(sqrt(49));
}
7
Mfano
Unataka kufanya hesabu za logarith sasa unataka kujuwa log ya 45
import 'dart:math';
void main()
{
print(log(25));
}
3.2188758248682006
Kuna mengi unaweza kuyapata kwenye math library. Kwa kuwa umeshajuw ajinsi ya kuitumia unaweza kuitafuta kupitia website ya dart, link yake utaipata kwenye somo la kwanza.
Mwisho:
Katika somo linalofuata tutakwenda kuziona method nyingine ambazo zinafanya kai kwenye list data type.