1. Ifraad.

-    Ni aina ya Hijja amapo Hajj anavaa Ihram kwa nia ya kufanya Hijjah tu bila ya Umrah. 

-    Huanza kwa Talbiya; “Allaahumma labbaykal-Hijja” – ‘Nimeitika kwa Hijjah’

-    Hajj huvaa Ihram mpaka amalize matendo yote ya Hija mwezi 10, Dhul-Hijjah.

-    Hajj halazimiki kuchinja siku ya mwezi 10, Dhul-Hijah. 

 

  1. Qiran.

-    Ni aina ya Hija ambapo Hajj hunuia kufanya Hija na Umrah pamoja.

-    Hajj huitika kwa Talbiya; “Allaahumma labbaykal-Hijja wal-Umrata” – ‘Nimeitika kwa Hijjah na Umrah.’

 

-    Hajj huwa katika Ihram mpaka alenge mawe minara mitatu, atufu Tawaful-Ifaadha na kunyoa mwezi 10, Dhul-Hijjah.

 

-    Hajj analazimika kuchinja mnyama.

-    Aina hii ya Hija hufanywa na wakazi wa Makka na wale waliokuja na wanyama.

 

  1. Tamattu.

-    Ni aina ya Hijah ambapo Hajj hunuia kufanya Umrah tu, kwa kuitika; “Allaahumma labbaykal-Umrah” – ‘Nimeitika kwa Umrah.’

 

-    Hajj huvua Ihram baada ya kufanya matendo yote ya Umrah na kunyoa na kuwa huru na miiko ya Ihram.

 

-    Hajj huvaa tena Ihram siku ya mwezi 8, Dhul-Hija na kuitika; “Allaahumma labbaykal-Hijjah” – ‘Nimeitika kwa Hijjah.’

 

-    Hajj atavua tena Ihram baada ya kutupa mawe na kunyoa mwezi 10, Dhul-Hija.

-    Hajj atalazimika kuchinja mnyama siku ya mwezi 10, Dhul-Hija kwa kununua mnyama kama hakuja nayo. Qur’an (2:196).


-    Aina hii ya Hija ni bora na nafuu kwa wanaotoka mbali na hawana wanyama wa kuchinja