- Funga za Kafara.
- Ni funga anazolazimika muislamu kufunga ili ziwe kitubio au fidia baada ya kutenda kosa fulani.
- Aina za funga za kafara.
- Kufunga miezi miwili mfululizo kwa muislamu aliyemuua mtu kwa bahati mbaya na akakosa mali ya kulipa fidia.
Rejea Qur’an (4:92).
- Kufunga miezi miwili mfululizo kwa muislamu aliyemsusa mkewe kwa kumfananisha na mama mzazi wake.
Rejea Qur’an (58:1-4).
- Kufunga siku tatu mfululizo kama kafara kwa muislamu aliyevunja kiapo.
Rejea Qur’an (5:89).
- Kufunga miezi miwili mfululizo kwa mume na mke waliofanya jimai (tendo la ndoa) mchana wa mwezi wa Ramadhani.
- Kufunga kama kitubio cha muislamu aliyewinda na hali yuko katika Ihram.
- Idadi ya siku inategemea na thamani ya kile alichokiua (alichokiwinda).
- Kama hana uwezo wa kufunga, atatoa fidia ya mbuzi au kondoo.
Rejea Qur’an (5:95).
- Kufunga siku 10, tatu akiwa Makkah na 7 baada ya kurejea nyumbani kwa muislamu aliyevunja miiko ya Ihram.
- Kama hana uwezo wa kufunga, atafidia kwa kuchinja mbuzi au kondoo.
Rejea Qur’an (2:196).